• HABARI MPYA

    Friday, June 13, 2014

    PIGO LINGINE ITALIA...SHAVU KA KUSHOTO TEGEMEO AZZURI LAUMIA

    BEKI wa kushoto wa Italia, Mattia De Sciglio ameondolewa kwenye mchezo wa ufunguzi wa Kundi D dhidi ya England mjini Manaus kesho kutokana na kuwa majeruhi.
    Habari hizo ni pogo kwa kocha wa Azzurri, Cesare Prandelli kwa kikosi chake wakati kesho anaanza kampeni za Kombe la Dunia.
    beki huyo wa AC Milan mwenye umri wa miaka 21, aliumia misuli jana mazoeini na kupelekwa hospital kwa ajili ya kuanyiwa vipimo vya MRI ili kujua ukubwa wa tatizo lake.
    Nje: Mattia De Sciglio ataukosa mchezo wa kwanza wa Italia dhidi ya England Kombe la Dunia

    "Beki Mattia De Sciglio, baada ya mazoezi leo (jana) huko Portobello (Mangaritiba), ameumia misuli ya mguu wake wa kushoto,"amesema daktari wa  Italia, Enrico Castellacci.
    Prandelli anatarajiwa kuziba pengo la De Sciglio kwa kumpanga beki wa Inter Milan, Andrea Ranocchia ni mchezaji wa akina kwenye Fainali hizi za Brazil.
    The Azzurri inaweza kubadilisha wachezaji kikosini make kutoka orodha ya awali iliyowasilisha kwa ajili ya michuano hiyo saa  24 kabla ya kucheza mechi yao ya kwanza.
    De Sciglio ameondolewa kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi D lakini anatarajiwa kuwa fiti kwa mchezo na Costa Rica Juni 20.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIGO LINGINE ITALIA...SHAVU KA KUSHOTO TEGEMEO AZZURI LAUMIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top