// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); IRAQ HUDU AFARIKI DUNIA, KUZIKWA KESHO DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE IRAQ HUDU AFARIKI DUNIA, KUZIKWA KESHO DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, June 13, 2014

    IRAQ HUDU AFARIKI DUNIA, KUZIKWA KESHO DAR

    Na Asha Said, DAR ES SALAAM
    BONDIA wa zamani wa ngumi za kulipwa nchini, Iraq Hudu 'Kimbunga'  amefariki dunia jana mjini Dar es Salaam akiwa ana umri wa miaka 49, baada ya kuugua kwa muda mfupi.
    Akizungumza Dar es Salaam leo, dada wa marehemu Tiba Takadir, amesema kwamba
    Hudu amefariki jana majira ya saa 11 ya alfajiri kwenye hospitali ya Hindu Mandal, alikokuwa amelazwa. Takadir, alimesema kuwa mazishi ya Hudu yatafanyika kesho Jumamosi kwenye makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.
    Alisema kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ini na figo kutofanya kazi, ambapo 

    vilimsumbua kwa muda mchache kabla ya kufariki kwake.
    "Marehemu alilazwa hospitali Hindu Mandal siku tatu zilizopita, ambapo majuzi jioni 
    alizidiwa na jana asubuhi kukutwa na umauti.
    Hudu amezaliwa mwaka 1965 Ujiji Kigoma, na kupata elimu ya msingi mkoani humo na baadae kuja Dar es Salaam ambapo alimaliza shule ya Sekondari na baadae kuanza shughuli za ngumi katika miaka ya 1990 mpaka miaka ya 2000 alipoacha.
    Marehemu ameacha watoto watatu, ambao ni Daniel alikuwa akitarajia kufunga ndoa Juni 20, 
    wakati mtoto mwingine Msawila ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita. 
    Maandalizi ya msiba yanaendelea nyumbani kwa marehemu Buguruni Lozana Dar es Salaam 
    ambapo kesho saa 7, atazikwa Kisutu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: IRAQ HUDU AFARIKI DUNIA, KUZIKWA KESHO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top