// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BIN SLUM WAICHUKUA TIMU YA PILI LIGI KUU, WAMWAGA MAMILIONI YA UDHAMINI STAND UNITED - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BIN SLUM WAICHUKUA TIMU YA PILI LIGI KUU, WAMWAGA MAMILIONI YA UDHAMINI STAND UNITED - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, June 13, 2014

    BIN SLUM WAICHUKUA TIMU YA PILI LIGI KUU, WAMWAGA MAMILIONI YA UDHAMINI STAND UNITED

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KAMPUNI ya Bin Slum Tyres Limited imeingia Mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja wenye thamani ya Sh Miliomi 50 na klabu mpya katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Stand United ya Shinyanga leo.
    Uongozi wa Stand United na Bin Slum Tyres umesaini Mkataba huo mchana wa leo barabara ya Samora, Dar es Salaam mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stepehen Masele ambaye pia ni Mbunge wa Shinyanga Mjini.
    Katika Mkataba huo, Stand United watavaa jezi zenye nembo ya matairi ya Double Star Tire yanayosambazwa na kampuni ya Bin Slum katika mechi zake zote msimu wa 2014-2015.
    Mkurugenzi wa kampuni ya Bin Slum Tyres Limited, Nassor Bin Slum kulia akitiliana saini fomu za mikataba na Mwenyekiti wa Stand United, Amani Vincent kushoto leo mjini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele. na Nyuma ni Mwanasheria wa DStand United.  

    Aidha, mabango ya Double Star pia yatabandikwa katika mechi za Uwanja wa nyumbani, Kambarage mkoani Shinyanga za timu hiyo.
    Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 2000 kwa mkoa wa Shinyanga kuwa na timu katika Ligi Kuu baada ya kuteremka Kahama United, kufuatia kupanda kwa Stand United msimu huu.
    Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo, Bin Slum amesema kwamba lengo la kuingia mkataba wa udhamini na timu hiyo ni kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
    “Rais wetu kipenzi, Jakaya Kikwete alishauri makampuni na wadau wazisaidie na timu ndogo pia ili kuziinua, badala ya kuelekeza nguvu zao kwa timu kubwa pekee, ambazo tayari zina vyanzo vya kiuchumi,”alisema.
    Bin Slum amesema pia pamoja na kuitikia wito huo wa rais JK, lakini pia mkoa wa Shinyanga ni mkubwa ambao anaamini anaweza akanufaika kibiashara kupitia udhamini wake Stand United.
    Wanabadilishana fomu za mikataba
    Wanatia saini fomu za mikataba
    Makabidhiano ya jezi
    Bin Slum katika uzi wa Stand United

    Mwenyekiti wa Stand United, Amani Vincent amesema kwamba anashukuru kwa udhamini huo na anaamini utawasaidia kufanya vizuri katika Ligi Kuu.
    “Udhamini huu ni faraja kwetu, utatusaidia kuwa na maandalizi mazuri kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu, na pia itatusaidia kufanya vizuri katika Ligi Kuu,”amesema.
    Kwa upande wake, Mbunge wa Shinyanga Mjini, Masele amesema ameikabidhi basi dogo timu hiyo aina ya Coaster na kuahidi kuendelea kuwa nayo bega kwa bega ili iweze kumudu mikiki ya Ligi Kuu.
    Naibu Waziri huyo aliyesaidia mno harakati za timu hiyo kupanda Ligi Kuu, amewaomba wadau wengine wa mkoa wa Shinyanga kuisapoti timu hiyo ili iwe imara na kutoa ushindani katika Ligi Kuu.
    Kwa Bin Slum Tyres Limited, Stand United inakuwa timu ya pili ya Ligi Kuu kwao kuidhamini baada ya Mbeya City ya Mbeya waliyoingia nayo Mkataba wa miaka miwili hivi karibuni.
    Mkataba wa Mbeya City ambao wao watatangaza betri za RB zinazosambazwa na kampuni hiyo pia, una thamani ya Sh. Milioni 360 kwa miaka hiyo miwili.
    Awali ya hapo, Bin Slum walikuwa wanaifadhili Coastal Union ya Tanga kwa miaka kadhaa kabla ya kujitoa mwishoni mwa msimu huu, baada ya kukerwa na uongozi wa sasa wa mabingwa hao wa Ligi Kuu 1988.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BIN SLUM WAICHUKUA TIMU YA PILI LIGI KUU, WAMWAGA MAMILIONI YA UDHAMINI STAND UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top