// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); DAU LA MAXIMO LAIHENYESHA YANGA, MANJI ASEMA ‘ATAKUFA NAYE’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE DAU LA MAXIMO LAIHENYESHA YANGA, MANJI ASEMA ‘ATAKUFA NAYE’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, June 02, 2014

    DAU LA MAXIMO LAIHENYESHA YANGA, MANJI ASEMA ‘ATAKUFA NAYE’

    Na Renatus Mahima, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mbrazil Marcio Maximo, aliyekuwa kocha wa timu ya taifa (Taifa Stars), muda wowote atatua nchini na kusaini mkataba wa kukinoa kikosi cha Yanga katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, imefahamika.
    Uongozi wa Yanga katika mkutano mkuu wa dharura wa wanachama iiliofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini hapa jana, umesema umekuwa na mazungumzo ya muda mrefu na kocha huyo ili achukue kandarasi ya kuinoa timu yao.
    Atakuja? Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Marcio Maximo anatakiwa na Yanga SC

    "Tunapenda kuwaataarifu wanachama wa Yanga kwamba tuna mpango wa kumleta Maximo kuifundisha timu yetu msimu ujao. Tumekuwa  na mazungumzo naye kwa miezi miwili sasa tukimwomba apungumze kidogo mshahara," amesema Yusuph Manji, Mwenyekiti wa Yanga.
    "Zoezi la usajili linakwenda vizuri. Hatusajili wachezaji wengi kwa sababu kikosi chetu cha msimu uliopita ni kizuri ndiyo tukaifunga hadi Al Ahly ya Misri. Tunachokifanya kwa sasa ni kurekebisha maeneo ambayo tumebaini kuwa na upungufu.
    "Wachezaji wote wanasajiliwa makao makuu ya klabu ili kuepuka matatizo ambayo yamejitokeza huko nyuma," amesema zaidi kiongozi huyo.
    Maximo, raia wa Brazil aliiongoza Taifa Starsb kwa mafanikio makubwa akisifika kama 'mhamasishaji' kutokana na Watanzania wengi kuingia viwanjani kuiona timu yao ya taifa ikicheza dhidi ya timu mbalimbali.
    Hamasa ya Watanzania kuishangilia ilianza kupungua baada ya kuondoka kwa kocha huyo na mikoba yake kuchukuliwa na Jan Poulsen ambaye baadaye arithiwa na Mdenmark mwenzake Kim Poulsen aliyetimuliwa mwanzoni mwa mwaka huu.
    Taifa Stars kwa sasa iko chini ya Mholanzi Mart Nooij na Yanga haina kocha mkuu baada ya kuondoka kwa Mholanzi Hans van der Pluijm Aprili mwaka huu.
    Aidha, katika mkutano huo wanachama wamepitisha kuingizwa kwa kipengele katika Katiba ya Yanga kinachotaka klabu hiyo iwe na Kamati ya Maadili kama ilivyoagizwa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka (TFF) Desemba mwaka jana.
    Kipengele kilichopitishwa kinasema: "Kutakuwa na Kamati nya Maadili itakayokuwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe watatu watakaoteuliwa na Kamati ya Utendaji na muda wao hautazidi mwaka mmoja. Mwenyekiti lazima na taaluma ya sheria."
    "Kazi za chombo hiki zitasimamiwa na Katiba ya Yanga na Kanuni za Maadili za Yanga na endapo hazitajitosheleza, Kanuni za Maadili za TFF zitatumika ipasavyo.
    "Rufaa zote kutoka Kamati ya Maadili zitasikilizwa na Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF."
    Aidha, wakati Mwenyekiti wa Yanga akitengua kauli yake ya kutowania tena uongozi, uchaguzi mkuu wa klabu hiyo sasa umepangwa kufanyika Juni 15 mwakani.
    Wanachama wa Yanga katika mkutano mkuu wa dharura wa marekebisho ya Katiba kwenhye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini hapa leo, wamekubaliana uchaguzi mkuu wa klabu hiyo ambao awali ulikuwa umepangwa kufanyika Juni 15 mwaka huu ufanyike mwakani ili kupishya shughuli mbalimbali za maendeleo ya klabu hiyo ikiwamo marekebisho ya Katiba na michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
    Novemba mwaka jana, Manji alitangaza kutowania tena uongozi ndani ya klabu hiyo ili kupisha watu wengine waiongoze klabu hiyo kongwe nchini katika kile alichokieleza kuwa kutimiza matakwa ya demokrasia.
    Lakini, baada ya ajenda kuu ya mkutano mkuu wa jana kuingiza kipengele cha kuunda Kamati ya Maadili ya Yanga kama ilivyoagizwa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) Desemba mwaka jana, wanachama wa Yanga katika kujadili mengineyo waliamua kuwaondoa mkutanoni kwa muda wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo ili kujadili kauli yao ya kutowania tena uongozi.
    Baada ya hoja hizo kujadiliwa huku wanachama mbalimbali akiwamo 'mzungu' Javet Peytov mwenye kadi ya uanachama Na. 009472, wakisimama na kuchagia, wajumbe hao walilazimika kufuta kauli hiyo na kurudhia kuwania tena uongozi katika uchaguzi mkuu ujao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DAU LA MAXIMO LAIHENYESHA YANGA, MANJI ASEMA ‘ATAKUFA NAYE’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top