• HABARI MPYA

    Sunday, September 01, 2013

    ROONEY HATARINI KUWAKOSA LIVERPOOL LEO, AUMIA KICHWA MAZOEZINI NA KUFUNGWA BANDEJI

    IMEWEKWA SEPTEMBA 1, 2013 SAA 11:14 ALFAJIRI
    MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amezalisha hofu Manchester United baada ya kuumia kichwa jana asubuhi na sasa kuna wasiwasi akaukosa mchezo wa leo dhidi ya Liverpool.
    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa England aliumia kichwa mazoezini asubuhi na aliondoka Uwanja wa mazoezi wa timu hiyo, Carrington HQ akiwa amefungwa bandeji iliyozunguka kichwa.
    Committed: Waynre Rooney (right) challenges Ashley Cole after coming on as substitute in Monday's 0-0 draw with Chelsea
    Ameumia: Wayne Rooney (kulia) akipambana na Ashley Cole katika mchezo dhidi ya Chelsea JUmatatu

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 yuko shakani sasa kucheza Anfield leo na hatima yake itaamuliwa na madaktari wa timu hiyo.
    Rooney alicheza soka ya nguvu United ikimenyana na Chelsea Jumatatu na kuondoa shaka juu ya mustakabali wake Old Trafford.
    Selection problem: David Moyes' team selection has been hit by Rooney's head injury
    Kichwa kinamuuma: Kocha David Moyes amepata pigo kwa Rooney kuumia kichwa

    Baada ya mechi hiyo, kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alimtaka mshambuliaji huyo kuweka wazi ndani ya saa 48 kama anabaki au anataka kuondoka, lakini Rooney alijibu kwa kuweka ujumbe kwenye ukurasa wake wa Facebook amefurahishwa na mapokezi aliyopewa na mashabiki katika mchezo huo.
    Fans' favourite: The Old Trafford faithful applauded Rooney after the Chelsea game for his display
    Kipenzi cha mashabiki: Rooney amefurahia mapokezi ya mashabiki Old Trafford katika mechi na Chelsea

    Sasa mkonwe Ryan Giggs anaweza kuchukua nafasi ya Rooney katika mchezo wa leo, akicheza sambamba na Danny Welbeck na Robin van Persie katika safu ya ushambuliaji. Mchezaji anayetakiwa na Tottenham, Javier Hernandez pia amekuwa akifanya mazoezi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ROONEY HATARINI KUWAKOSA LIVERPOOL LEO, AUMIA KICHWA MAZOEZINI NA KUFUNGWA BANDEJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top