• HABARI MPYA

    Tuesday, September 03, 2013

    MABINGWA WA KENYA TUSKER FC WATUA DAR ALHAMISI KUKIPIGA NA SIMBA NA YANGA TAIFA

    Na Prince Akbar, IMEWEKWA SEPTEMBA 2, 2013 SAA 6:39 MCHANA
    MABINGWA wa Kenya, Tusker FC wanawasili nchini Alhamisi kwa ajili ya michezo miwili ya kujipima nguvu dhidi ya mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC Jumamosi na Simba SC Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Mechi hizo zimeandaliwa na Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) na Yanga SC wanataka kuutumia kwa ajili ya maandalizi ya michezo yao ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wiki ijayo Nyanda za Juu Kusini.
    Yanga SC itacheza mechi mbili mfululizo Mbeya wiki ijayo dhidi ya timu za huko, ikianza na Mbeya City Septemba 14 na baadaye Prisons Septemba 18, Uwanja wa Sokoine mjini humo.
    Wanakuja; Mabingwa wa Kenya, Tusker FC wanakuja kucheza na Simba na Yanga 

    Tarayi Yanga SC imecheza mbili za Ligi Kuu msimu huu mpya Dar es Salaam dhidi ya Ashanti United waliyoshinda 5-1 na Coastal Union waliyotoka nayo sare ya 1-1.
    Tusker nayo itautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yake ya mechi za Ligi Kuu ya Kenya inayoendelea nchini humo.
    Kadhalika Simba SC watautumia mchezo wao na Tusker kwa maandalizi ya mechi zake za Ligi Kuu wiki ijayo.
    Baada ya mechi za mbili mikoani, Tabora dhidi ya Rhino Rangers waliyotoka nayo sare ya 2-2 na JKT Oljoro waliyoshinda 1-0 Arusha, Simba SC watacheza mechi zaidi ya tano Dar es Salaam kuanzia wiki ijayo, wakianza na Mtibwa Sugar Septemba 14. 
    Kwa kuwa Tusker ni mabingwa wa Kenya na timu yenye uzoefu wa kucheza Tanzania, wazi Simba na Yanga zitapata mechi nzuri za kujipima.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MABINGWA WA KENYA TUSKER FC WATUA DAR ALHAMISI KUKIPIGA NA SIMBA NA YANGA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top