• HABARI MPYA

    Tuesday, June 11, 2013

    WAALGERIA KUCHEZESHA TAIFA STARS, IVORY COAST

    Mungu ibariki Taifa Stars
    Na Boniface Wambura, IMEWEKWA JUNI 11, 2013 SAA 1:00 USIKU
    SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeteua waamuzi kutoka Algeria kuchezesha mechi kati ya Taifa Stars na Ivory Coast itakayofanyika Jumapili saa 9:00 Alasiri kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Waamuzi hao watakaochezesha mechi hiyo ya kundi C kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil wataongozwa na Charef Mehdi Abid atakayepuliza filimbi. Atasaidiwa na Hamza Hammou na Bouabdallah Omari wakati mezani atakuwa Sofiane Bousseter.
    Abdi na wezake wanatarajiwa kutua nchini Ijumaa (Juni 14 mwaka huu) saa 12 asubuhi kwa ndege ya Shirika la Usafiri wa Anga la Misri. Mtathmini wa waamuzi ni Athanase Nkubito kutoka Rwanda ambaye atatua nchini Ijumaa (Juni 14 mwaka huu) saa 12 jioni kwa ndege ya RwandAir.
    Kamisaa wa mechi hiyo ni Bernard Mfubusa kutoka nchini Burundi ambapo atawasili nchini Ijumaa (Juni 14 mwaka huu) saa 3.35 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways. Maofisa wote hao wa mechi hiyo watarejea makwao Jumatatu (Juni 17 mwaka huu).
    Wakati Ivory Coast iliifunga Gambia 3-0 Jumamosi, Stars ilifungwa 2-1 na wenyeji Jumamosi katika michezo iliyopita ya Kundi C kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia Brazil mwakani. 
    Stars ipo nafasi ya pili mbele ya Morocco yene pointi tano sasa, wakati Ivory Coast wanaongoza kwa pointi zao 10, zikiwa zimesalia mechi mbili mbili kumaliza hatua ya makundi. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: WAALGERIA KUCHEZESHA TAIFA STARS, IVORY COAST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top