• HABARI MPYA

    Monday, June 10, 2013

    REAL MADRID SASA IMEAMUA...YASEMA ITAVUNJA REKODI YA DUNIA KWA BALE

    IMEWEKWA JUNI 10, 2013 SAA 3:30 ASUBUHI
    MWANASOKA bora wa zamani wa dunia, Zinedine Zidane amesema Real Madrid watavunja rekodi ya dunia ya usajili kwa kumsaini Gareth Bale.
    Winga huyo wa Tottenham amekuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa kuhamia kwa wababe hao wa Hispania katika Jiji la Madrid walio tayari kutoa Pauni Milioni 85.
    Hiyo itavunja rekdi ya usajili ghali kwa mchezaji ya Pauni Milioni zilizotumika kumsaini aliyekuwa mchezaji wa Manchester United, Cristiano Ronaldo miaka minne iliyopita.
    Target: Tottenham winger Gareth Bale is on Real Madrid's radar and could cost £85million
    Anatakiwa: Winga wa Tottenham, Gareth Bale yupo kwenye rada za Real Madrid kwa Pauni Milioni 85

    "Mazungumzo kuhusu Gareth Bale si ya kushitukiza," amesema Zidane, ambaye ni Mkurugenzi wa Michezo Madrid na kuongeza watapanda dau zaidi iwapo itatokea klabu ya kutaka kushindana nao kuwanai saini ya mchezaji huyo.
    "Kuna klabu nne au tano kwa sasa ambazo zina uwezo wa kifedha kumsajili, lakini si kwa kuvunja rekodi ya ada ya uhamisho kama hivyo,"aliongeza.
    Man with the plan: Zinedine Zidane (centre) admits it will take a big bid to sign Bale this summer
    Mtu wa mipango: Zinedine Zidane (katikati) amesema atapambana kumsaini Bale majira haya ya joto

    Dau hilo kubwa haitakuwa rahisi kwa Spurs kukataa kumuuza na bosi wa Bernabeu, Florentino Perez amemlenga nyota huyo wa Wales kama chauo lake kuu.
    Bale anaweza kuchukuliwa Madrid akazibe nafasi ya Ronaldo ambaye amekuwa akihusishwa na kurejea Old Trafford.
    Wakati huo huo, Viongozi wa Juventus wamefanya mazungumzo na Madrid kuhusu Gonzalo Higuain jana. Wataliano hao wanataka kuipiku Arsenal kumsaini Muargentina huyo anayeuzwa Pauni Milioni 20, lakini wameambiwa dili hilo itabidi lisubiri hadi Carlo Ancelotti apewe mikoba ya ukocha.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: REAL MADRID SASA IMEAMUA...YASEMA ITAVUNJA REKODI YA DUNIA KWA BALE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top