• HABARI MPYA

    Tuesday, June 11, 2013

    MAN CITY YAKAMILISHA USAJILI WA JESUS NAVAS

    IMEWEKWA JUNI 11, 2013 SAA 2:50 USIKU
    KIUNGO wa Hispania, Jesus Navas amekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 15 kutoka Sevilla kwenda Manchester City, na kusema Ligi Kuu ya England ni bora kwake kupiga hatua ya maendeleo kama mchezaji.
    City imethibitisha dili hilo, na Navas anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na klabu hiyo majira haya ya joto baada ya kiungo wa Shakhtar, Fernandinho aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 30 wiki iliyopita.
    Winga huyo wa kulia mwenye umri wa miaka 27 amekamilisha vipimo vya afya Jijini New York, ambako yuko na kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kwa maandalizi ya mechi na Ireland na atajiunga na kikosi cha City baada ya Kombe la Mabara.
    Got him: Claudio Reyna and Navas after the Spaniard put pen to paper
    Wamempata: Claudio Reyna na Navas baada ya Mspanyola huyo kumwaga wino kwenye karatasi za City
    Arrival: Navas signs from Sevilla for £15million
    Amewasili: Navas amesaini kutoka Sevilla kwa Pauni Milioni 15
    Navas
    Navas hadi sasa ameichezea mechi 23 Hispania, akiisaidia nchi yake kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2010 na Euro miaka miwili iliyopita.
    Navas alikutana na kiungo wa zamani wa City, Claudio Reyna, aliyechaguliwa hivi karibuni kuwa Mkurugenzi wa Michezo wa New York City FC, Jijini the New York kukamilisha usajili wake.
    Experience: Navas has 23 caps for Spain, and played in the 2010 World Cup and Euro 2012 wins
    Mzoefu: Navas ameichezea mechi 23 Hispania, na alishinda mataji ya Kombe la Dunia 2010 na Euro 2012
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MAN CITY YAKAMILISHA USAJILI WA JESUS NAVAS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top