IMEWEKWA JUNI 9, 2013 SAA 3:40 USIKU
MTENDAJI Mkuu wa Borussia Dortmund amesema kwamba mshambuliaji Robert Lewandowski hatauzwa kwa Bayern Munich majira haya ya joto.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Poland, mwenye umri wa miaka 24, alisemekana kuhamia timu nyingine Ujerumani, kwa wapinzani wa Dortmund, Bayern lakini sasa Manchester United wanaweza kumnyakua.
Mchezaji mwenzake Mario Gotze alizua tafrani alipokubali kujiunga na washindi hao wa Ligi Kuu ya Ujerumani kwa msimu ujao na Lewandowski alitarajiwa kumfuata.
Anaondoka: Robert Lewandowski hataruhusiwa kusaini Bayern Munich majira haya ya joto
CEO wa Dortmund alisema kama ilivyoripotiwa na Bild: "Robert Lewandowski hatahamia FC Bayern mwaka 2013. hiyo ni mwisho. Tumemuambia Robert na wakala wake sasa,".
United, ambao wanammezea mate Lewandowski kwa muda mrefu, sasa watatazamiwa kupambana kumpata mpachika mabao huyo kama sasa atapenda kuhamia klabu ya nje ya Bundesliga.
Anayetakiwa kwa muda mrefu: Mshambuliaji wa Poland, anatakiwa na Manchester United majira haya ya joto
Chelsea pia inaweza kuhamishia ndoana zake kwa Lewandowski wakiwa sokoni hivi sasa wanasaka mshambuliaji na kwa sasa wamewalenga Stevan Jovetic, Edinson Cavani na Hulk.
Wanaondoka: Huku Mario Gomez (kushoto) akitarajiwa kuhama Bayern Munich na Wayne Rooney pia ameripotiwa kutaka kuhama Manchester United, Lewandowski ndiye mbadala wao sahihi.