• HABARI MPYA

    Thursday, June 13, 2013

    BARCELONA YATAKA KUMSAJILI TORRES AWE SUPER SUB CAMP NOU

    IMEWEKWA JUNI 13, 2013 SAA 6:00 USIKU
    HAWATOSHI Messi na Neymar peke yao kuongoza safu ya ushambuliaji, Barcelona imeripotiwa kutaka kumnunua mshambuliaji Fernando Torres.
    Gazeti la kila siku la Catalan, Sport limeandika kwamba Barcelona inataka kutoa Pauni Milioni 17 (zaidi ya Euro Milioni 20) kumnunua mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anayekipiga Chelsea.
    Read all about it: Catalan daily Sport claim that Barcelona are considering a 20m Euro bid for Torres
    Soma yote juu ya hii: Gazeti la michezo la kila siku la Catalan, Sport limeandika kwamba Barcelona inataka kumnunua kwa Euro Milioni 20 Torres

    REKODI YA MABAO YA TORRES

    MsimuMabao
    2012-1322
    2011-1211
    2010-1110
    2009-1022
    2008-0917
    Pamoja na hayo, Torres hatakuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza bali atakuwa anatokea benchi kama super-sub.
    Matumani ni kwamba, Torres atatengeneza uzito sawa na aliokuwa nao Henrik Larsson, ambaye alikuwa kipenzi cha mashabiki enzia zake Nou Camp kwa kufanya vitu adimu akitokea benchi hususan alipotoa pasi za mabao yote Barcelona ikishinda 2-1 dhidi ya Arsenal katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2006.
    Lakini Sport limemsifia Torres ni mshambuliaji wa uhakika ambaye anaweza kufunga mabao kati ya 20 na 25 kwa mwaka.
    Glory goal: Torres scored against Barcelona at the Nou Camp in the Champions League semi-finals last year
    Bao la ushindi: Torres alifunga dhidi ya Barcelona Uwanja wa Nou Camp katika Nusu Fainali ya Mabingwa mwaka jana
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BARCELONA YATAKA KUMSAJILI TORRES AWE SUPER SUB CAMP NOU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top