• HABARI MPYA

    Saturday, April 06, 2013

    YANGA SC WAINGIA KAMBINI KUIWEKEA AKILI SAWA JKT OLJORO

    Kikosi cha Yanga

    Na Baraka Kizuguto
    KIKOSI cha tmu ya Young Africans kimeingia kambini katika hosteli zilizopo makao makuu ya klabu mitaa ya Twiga/Jangwnai jana jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom unaofuata dhidi ya timu ya JKT Oljoro siku ya jumatano katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
    Young Africans ambayo inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya VPL kwa kuwa na pointi 49 na mabao 37 ya kufunga, itashuka dimbani siku ya jumatano kuhakikisha inaibuka na ushindi katika mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa mgumu zaidi kwani kila timu inahitaji pointi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.
    Katika mchezo wa awali wa mzunguko wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 1-0  bao lililofungwa na mlinzi kati wa kimataifa Mbuyu Twite ambaye pia anachezea timu ya Taifa ya Rwanda Amavubi.
    Kocha Brandts amesema kikosi chake kipo katika hali nzuri kuelekea mchezo wa jumatano, kwani wachezaji wote ni wazima wa afya, kiakili/kifikra na morali ni ya hali ya juu katika kuhakikisha timu inapata ushindi katika mechi ya jumatano.
    Kila mchezo kwetu tunautazama kama fainali, kufuatia na timu zote za Ligi Kuu katika mzunguko wa pili kubadilika, kila timu inahitaji ushindi, inahitaji kuonyesha ina uwezo lakini kwa kua sisi ni bora, mwisho wa siku naamini timu yangu itaibuka na ushindi alisema 'Brandts'
    Yanga imebakisha michezo mitano (5) ili kumalizika kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom huku ikihitaji kushinda japo michezo miatatu mfululizo ili iweze kutangazwa mabingwa wapya wa VPL 2012/2013.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: YANGA SC WAINGIA KAMBINI KUIWEKEA AKILI SAWA JKT OLJORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top