• HABARI MPYA

    Saturday, April 06, 2013

    KOCHA JKT RUVU ATUPIWA VIRAGO INGAWA NI MADUDU YA UONGOZI YAMEIPONZA TIMU KUFANYA VIBAYA

    Nje; Charles Kilinda ametimuliwa JKT Ruvu

    Na Mwandishi Wetu
    KLABU ya JKT Ruvu ya Pwani iliyohamishia maskani yake Dar es Salaam, imemfukuza kocha wake Charles Killinda na sasa ipo katika mchakato wa kusaka kocha mpya.
    JKT imemfukuza Kilinda aliyefanya kazi katika klabu hiyo tangu mwaka 2007, akirithi mikoba ya Freddy Felix Minziro, ambaye kwa sasa ni kocha Msaidizi wa Yanga.
    Sababu za kufukuzwa kwa kiungo huyo wa zamani wa Yanga katika klabu hiyo ni matokeo mabaya ya timu hiyo msimu huu, ambayo hata hivyo ukizama ndani unagundua hayasababishwi na kocha.
    Chanzo cha kufanya vibaya kwa JKT Ruvu msimu huu ni usajili mbovu na habari kutoka ndani ya timu hiyo zinasema kwamba ushauri wa kocha haukufuatwa katika zoezi hilo.
    “Kocha alipendekeza usajili wa wachezaji wengi vijana kutoka kikosi cha pili, lakini uongozi ukaamua kusajili ‘mafaza’ kutoka timu mbalimbali, ambao wameshindwa kuisaidia timu. Sasa wanamtoa kafara kocha kwa makosa yao wenyewe,”kilisema chanzo kutoka JKT Ruvu. 
    Kwa sasa, JKT Ruvu inashika nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza mechi 21.
    Kocha Msaidizi wa JKT Ruvu, Azishi Kondo hana sifa za kukaimu nafasi ya Kilinda, jambo ambalo litawalazimu Maafande hao kuajiri kocha mpya kabla ya kumenyana na Coastal Union ya Tanga katika mchezo wake ujao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KOCHA JKT RUVU ATUPIWA VIRAGO INGAWA NI MADUDU YA UONGOZI YAMEIPONZA TIMU KUFANYA VIBAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top