• HABARI MPYA

    Saturday, October 13, 2012

    NSA JOB AWATANGAZIA MAJANGA SIMBA SC LEO

    Nsa aliyebinuka tik tak mbele ya Juma Nyosso wa Simba, enzi hizo akiichezea Yanga. Leo atawafunga kweli Simba?

    Na Mahmoud Zubeiry, Tanga
    NSA Job, mshasmbuliaji wa Coastal Union ya Tanga amesema kwamba hakuna beki wa Simba anayeweza kumzuia asifunge bao katika mechi ya leo, kwa sababu wote anawajua.
    Nsa amewaahidi raha mashabiki wa Coastal Union leo, akisema kwamba dakika 90 ni nyingi mno kwake na haziwezi kumalizika bila kufunga hata bao moja.
    “Nawaahidi wapenzi na mashabiki wa Coastal furaha katika mechi yetu na Simba, nitawafunga lazima, kwa sababu hakuna beki wa kunizuia mimi kufanya hivyo, sijui wawe na bahati gani tu niwakose,”alisema Nsa.
    Nsa alisema kwamba kwa ujumla timu yao iko vizuri na nia yao msimu huu ni kufanya vizuri katika Ligi Kuu ili kuwakumbusha wakazi wa Tanga, enzi za Coastal iliyokuwa tishio katika soka ya Tanzania.
    “Simu ni timu ya kawaida sana, tunaijua vizuri, hakuna kipya pale na kwa kudhihirisha hilo, sisi tunawafunga kwenye mechi hii,”alisema Nsa.
    Nsa amewahi kucheza Simba msimu wa 2006, lakini akatemwa na kurejea Moro United kabla ya baadaye kusajiliwa Azam FC, Yanga, Villa Squad na msimu huu ametua Tanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: NSA JOB AWATANGAZIA MAJANGA SIMBA SC LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top