• HABARI MPYA

  Wednesday, October 31, 2012

  YANGA B WAITILIA UBANI YANGA A, WAYACHAPA KIDUDE MAKINDA YA MGAMBO


  Timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Yanga, imeifunga Mgambo JKT ya vijana pia, bao 1-0 katika mchezo wa utangulizi, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kabla ya kuanza kwa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baina ya kaka zao, Yanga A dhidi ya Mgambo JKT ya Handeni, Tanga. Bao hilo pekee lilitiwa kimiani na Clever Charles dakika ya 65.
  Zuberi Amiri wa Yanga B, akichuana na Charles Domayo wa JKT Mgambo

  Joseph Banda wa Yanga B (25) akipasua ukuta wa Mgambo

  Meshack Ramadhani wa Yanga kushoto akigombea mpira na beki wa Mgambo

  Banda akifumua shuti mbele ya mabeki wa Mgambo, mmoja akijaribu kuzuia

  Notikel Masasi wa Yanga B akiwa chini ya ulinzi wa mabeki wa Mgambo

  Kocha Ernie Brandts akifuatilia vipaji Yanga B ikicheza na Mgambo

  Notikel Masasi wa Yanga B, akichuana na mchezaji wa Mgambo

  Clever Charles, mfungaji wa bao la Yanga B leo, akiwa benchi baada ya kupumzishwa. Kulia kwake ni Said Manduta.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: YANGA B WAITILIA UBANI YANGA A, WAYACHAPA KIDUDE MAKINDA YA MGAMBO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top