RIO FERDINAND KUREJEA WEST HAM UNITED


Rio Ferdinand
Rio Ferdinand anaweza kurejea West Ham
West Ham inaweza kumpa ofa beki wa Manchester United, Rio Ferdinand, mwenye umri wa miaka 33, kurejea katika kumalizia soka yake katika klabu hiyo ya London atakapomaliza mkataba wake Old Trafford mwishoni mwa msimu ujao.
West Ham pia ina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Lokomotiva, Andrej Kramaric, mwenye umri wa miaka 21, ambaye amefunga mabao manane katika mechi 12za ligi, wakati akicheza kwa mkopo kutoka Dinamo Zagreb.

MAFAZA MAN CITY WAKERWA NA MFUMO WA MANCINI WAKIPIGWA 3-1 NA AJAX

Wachezaji kadhaa waandamizi Manchester City wamekerwa na mfumo wa kocha Roberto Mancini, katika kipigo chao chao mabao 3-1 walichokipata kutoka kwa Ajax juzi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Manchester City ipo karibu kumnasa Mkurugenzi wa Michezo wa zamani wa Barcelona, Txiki Begiristain ajiunge na klabu hiyo, baada ya mtu huyo mwenye umri wa miaka 48 kuzivutia pia klabu za Liverpool, Tottenham na Chelsea.
Nyota wa zamani wa Arsenal, Stewart Robson anaamini matatizo ya safu ya ulinzi ya The Gunners yatamalizwa kwa ushirkiano wa pamoja kati ya Kocha Arsene Wenger na Msaidizi wake, Steve Bould.
Kocha wa Aston Villa, Paul Lambert amesema hakujisikia vizuri kabisa wakati mashabiki wa Villa walipokuwa wakitaja jina lake akiwa bado kocha wa Norwich.
Coventry City imewataka mashabiki wake kuacha kuwakandia wachezaji wao kwenye Twitter wakati beki Jordan Clarke, mwenye umri wa miaka 20, akiwa anasumbuliwa na tukio la ubaguzi.