ADEBAYOR KUONDOKA SPURS

Mshambuliaji wa Tottenham, Emmanuel Adebayor, mwenye umri wa miaka 28, yu tayari kuondoka White Hart Lane kiasi cha miezi miwili tangu asajiliwe moja kwa moja kutoka Manchester City kwa dau la pauni Milioni 5.
Atletico Madrid inataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Javier Hernandez, mwenye umri wa miaka 24, ifikapo Januari iwapo wakimuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, Falcao - ambaye anatakiwa na Manchester City na Chelsea.
Beki wa Arsenal, Andre Santos, mwenye umri wa miaka 29, anaweza kurejea Uturuki, dlicha ya kutua Emirates mwaka jana tu, akitokea Fenerbahce kwa dau la pauni Milioni 6.2.

LEE CLARK AVUTIWA NA RAVEL MORRISON

Kocha wa Birmingham City, Lee Clark amemlinganisha kiungo Ravel Morrison na Paul Gascoigne baada ya kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 kuchezea dhidi ya Leicester akiwa kwa mkopo kutoka West Ham.
Ravel Morrison
Ravel Morrison amemvutia kocha wa Birmingham, Lee Clark
Beki wa Norwich, Sebastien Bassong, mwenye umri wa miaka 26, ameuelezea ushindi wa Jumamosi wa 1-0 dhidi ya Arsenal kwamba ni baab kubwa.
Juan Mata, mwenye umri wa miaka 24, amesema kutemwa kwenye kikosi cha Hispania cha sasa kutamfanya acheze vizuri zaidi Chelsea.
Arsene Wenger amesema kwamba Arsenal iliathiriwa na mfumo wake, katika kipigo cha 1-0 kutoka Norwich juzi, lakini anatarajia watazinduka Jumatano dhidi ya Schalke.
Alan Pardew anaamini timu yake, Newcastle watarejea cheche zao za msimu uliopita  baada ya kuanza kwa kusuasua kidogo msimu huu.
Kocha wa Chelsea, Roberto Di Matteo amekataa kubebwa kutokana na matokeo mazuri ya timu yake kwa sasa kwa sababu anaamini utafikia wakati watakutana na majaribu.
NICKY BUTT AREJEA MAN UNITED
Nyota wa zamani wa Manchester United, Nicky Butt, mwenye umri wa miaka 37, amerejea Old Trafford kama kocha wa vijana.