Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Soka Dar es Salaam
(DRFA), Juma Simba ‘Gadaffi’ (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo,
kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya uchaguzi
wa chama hicho. Simba amesema uchaguzi wa DRFA utafanyika Desemba 8, mwaka huu
na fomu za kugombea nafasi mbalimbali zitaanza kutolewa kesho. Novemba 4 hadi
8, Kamati yake itapitia fomu za walioomba uongozi, Novemba 9 hadi 13 utakuwa muda
wa pingamizi kwa wagombea, ambazo zitajadiliwa Novemba 14 hadi 16, wakati
Novemba 17 hadi 19 watatoa fursa ya kukata rufaa, ambazo zitasikilziwa Novemba
20 hadi 24 na baada ya hapo, Novemba 25 yatatangazwa majina ya wagombea
waliopitishwa. Tarehe hii mpya ya uchaguzi wa DRFA inaufanya usogeleane na uchaguzi wa TFF, ambao utafanyika pia Desemba.
|