• HABARI MPYA

    Monday, October 29, 2012

    BUNJAK ATUPIWA VIRAGO AZAM, KOCHA USHINDI AREJESHWA KAZINI


    Bunjak kulia akiwa na Kali Ongala na Daktari wa timu katika mechi ya juzi dhidi ya Simba
    Na Mahmoud Zubeiry
    KOCHA Mserbia wa Azam FC, Boris Bunjak amefukuzwa rasmi leo na sasa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Muingereza Stewart Hall anarudishwa kazini.
    Habari kutoka ndani ya Azam FC zimesema kwamba, sababu za kufukuzwa kwa Mserbia huyo ni kushuka kwa kiwango cha timu, hali iliyosababisha sasa ianguke hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
    Tayari Bunjak amekwishapewa haki zake zote na ataondoka Alhamisi, siku ambayo Stewart atawasili kuanza tena kazi Azam FC.
    Bunjak anaondoka Azam baada ya kuiongoza timu katika mechi 16, akifungwa nne tu, zote dhidi ya Simba ikiwemo ya juzi ya Ligi Kuu, waliyofungwa 3-1 na kutoa sare tatu.
    Bunjak mwenye leseni ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), alitua Azam, Agosti 7, mwaka huu akitokea FC Damac ya Saudia Arabia aliyoanza kuifundisha mwaka jana na kabla ya hapo alifundisha klabu kibao za kwao, zikiwemo FK Sloga Kraljevo, FK Javor Ivanjica, Crvena Zvezda Gnjilane, FK Radnicki Nis, FC Uralan Elista, FK Mladi Radnik, FK Crvena Zvezda Beograd, Al-Shaab, FK Hajduk Kula na Al-Nasr.
    Awali, Bunjak aliyezaliwa Novemba 17, mwaka 1954 ( miaka 57), alicheza soka katika klabu za FK Sloga (Kraljevo), FK Vozdovac (Beograd), FK Radnicki (Kragujevac), FK Olimpia (Ljubljana), FK Sumadija (Arandjelovac), FK Sloga (Kraljevo), FK Borac (Cacak) na FK Sloga (Kraljevo).
    Stewart alifukuzwa kwa kosa la kukaidi maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi ya klabu hiyo, kumpanga Mrisho Khalfan Ngassa katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya Yanga.
    Mserbia huyo anakuwa kocha wa tano kufukuzwa Azam, ndani ya miaka minne tangu ianze kucheza Ligi Kuu, 2008 baada ya Stewart, Mbrazil Neider dos Santos, Sylvester Marsh na Itamar Amorin, Mbrazil mwingine.
    Lakini Stewart angalau aliacha kumbukumbu ya taji na Medali Azam, baada ya kuiwezesha kutwaa Kombe la Mapinduzi Januari, kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Aprili, kabla ya kushika nafasi ya pili Kombe la Urafiki na Kagame miezi miwili iliyopita, mambo ambayo bila shaka yamemfanya afikiriwe tena.
    Stewart ana sifa ya kutokuwa mbinafsi na mwenye kuwaamini watu wa chini yake, kwa mfano namna ambavyo alikuwa akimpromoti Kali Ongala. Alimkuta Kali kama mchezaji, lakini kwa sababu ya umri kumtupa mkono, akashauriana naye awe Kocha Msaidizi na mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga, akakubali.
    Chini ya Stewart, Kali alikuwa akiachiwa timu aiongoze ili kumjengea kujiamini zaidi na mwezi uliopita aliachiwa timu kwenye Kombe la Urafiki, akaifikisha fainali, ambako ilifungwa na Simba kwa penalti kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.  

    WASIFU WA BORIS BUNJAK:
    JINA KAMILI: Boris Bunjak
    KUZALIWA: Novemba 17, 1954 (Miaka 57)
    KLABU ALIZOCHEZEA:
    1967- 1975: FK Sloga (Kraljevo)
    1975- 1978  FK Vozdovac (Beograd)
    1978- 1979  FK  Radnicki (Kragujevac)
    1979- 1980  FK Olimpia (Ljubljana)
    1980- 1981  FK  Sumadija (Arandjelovac)
    1981- 1985  FK  Sloga (Kraljevo)
    1985- 1986  FK  Borac (Cacak)
    1986- 1990  FK  Sloga (Kraljevo)
    KLABU ALIZOFUNDISHA:
    1990-1993:   FK Sloga (Kraljevo)
    1995-1996:   FK Javor (Ivanjica)
    1996-1997:   Crvena Zvezda (Gnjilane)
    1999:                      FK Radnicki (Nis)
    2000:                      FC Uralan Elista (Urusi)
    2000-2002:   FK Mladi (Radnik)
    2002-2004:   FK Crvena Zvezda (Beograd)
    2004:                      Al-Shaab (UAE)
    2005:                      FK Hajduk (Kula)
    2006-2007:   Al-Nasr (Oman)
    2009:                      Al Oruba Sur (Oman)
    2011:                      FC Damac (Saudi Arabia)
    2011:                      AL NASER (Oman)
      
    REKODI YA BORIS BUNJAK AZAM
    Azam 2-1 Polisi                   (BancABC)
    Azam 1-2 Simba B              (BancABC)
    Azam 8-0 Trans Camp        (Kirafiki)
    Azam 1-0 Prisons               (Kirafiki)
    Azam 2-0 Coastal Union     (Kirafiki)
    Azam 2-3 Simba SC           (Ngao ya Jamii)
    Azam 1-0 Kagera Sugar     (Ligi Kuu)
    Azam 2-2 Toto African        (Ligi Kuu)
    Azam 3-0 JKT Ruvu           (Ligi Kuu)
    Azam 1-0 Mtibwa Sugar     (Ligi Kuu)
    Azam 1-0 African Lyon       (Ligi Kuu)
    Azam 2-3 Simba SC           (Kirafiki)
    Azam 1-0 Polisi                  (Ligi Kuu)
    Azam 0-0       Prisons         (Ligi Kuu)                                      
    Azam 1-1 Ruvu Shooting    (Ligi Kuu)
    Azam 1-3 Simba                 (Ligi Kuu)
    Kocha ushindi na mataji anarudi, Stewart Hall

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BUNJAK ATUPIWA VIRAGO AZAM, KOCHA USHINDI AREJESHWA KAZINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top