• HABARI MPYA

    Sunday, October 28, 2012

    OKWI AJIBU TUHUMA SIMBA NA KUTENGENEZA UGALI WA MAANA MKATABA MPYA SIMBA

    Okwi

    Na Mahmoud Zubeiry
    MABAO mawili aliyofunga mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi jana katika mechi dhidi ya Azam FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana yanamaanisha mambo mawili makubwa kwake.
    Kwanza yamemsafisha mbele ya mashabiki wa timu hiyo, kufuatia tuhuma za aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Kassim Mohamed Dewji kwamba haitumikii kwa moyo safi klabu hiyo na pia yamepandisha thamani yake katika kipindi hiki cha mazungumzo ya kusaini mkataba mpya.
    Mzambia Felix Sunzu ndiye anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Simba SC, Sh. Milioni 5 na Okwi anayelipwa Sh. Milioni 2 anataka alipwe zaidi kwa sababu anaamini ndiye anayeibeba zaidi timu hiyo.
    Baada ya mechi ya jana, gumzo kubwa kwa mashabiki wa Simba lilikuwa ni bao la pili alilofunga Okwi- kwamba lilikuwa zuri mno na wanaamini hakubahatisha, kwa sababu amekuwa akifunga mabao kama hayo mara kadhaa.  
    Pamoja na hayo, katikati zilibuliwa tuhuma kwamba Okwi ana mapenzi na Yanga na amekuwa akiihujumu timu hiyo- huku habari nyingine zikisema anataka kwenda Azam.
    Okwi hakuwahi kuibuka kujibu tuhuma hizo, lakini shughuli yake ya jana ni sawa na majibu, kwani mabao hayo pamoja na kuidhuru Azam, lakini yameifanya Simba ijichimbie kileleni na kuwaacha wapinzani wao, Yanga.
    Okwi pia anawapelekea ujumbe viongozi wa Simba kwa mabao yake ya jana, waache kusikiliza maneno ya mitaani na kukumbuka wajibu wao kama viongozi kwa kujitofautisha na mashabiki.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: OKWI AJIBU TUHUMA SIMBA NA KUTENGENEZA UGALI WA MAANA MKATABA MPYA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top