• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 22, 2012

  BALOZI WA GLENMORANGIE AWASILI DAR

  Balozi wa kampuni ya Glenmorangie, Bwana Niel Hendriksz,akizungumza na Waandishi wa Habari katika hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam, zamani Kilimanjaro. 


  Balozi akikaribishwa kuzungumza na Meneja Masoko, Omari Salisbury

   
  Na Prince Akbar
  BALOZI wa kampuni ya Glenmorangie, Bwana Niel Hendriksz, amewasili leo hapa Dar es Salaam kwa ziara ya siku mbili ikiwa ni katika ziara yake ya siku tano katika ukanda wa Afrika Mashariki.
  Dhumuni ya ziara yake ni kuwazawadia wanywaji wa Glenmorangie pamoja na kuwaelimisha na kujenga uelewa kuhusu utumiaji wa vinywaji vya Glenmorangie katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
  Glenmorangie inafahamika kama kinywaji cha wiski pekee ya kutoka Skotland (Single Malt Scotch Whiskey) tamu na inayopendwa zaidi duniani. Ikiwa imejijengea umaarufu kama mojawapo ya wiski za awali kabisa, hasa kwa kuweza kuchanganya mbinu za kitamaduni pamoja na ugunduzi mpya wa kisasa kujitengenezea jina lake maarufu la ‘Unnecessarilly well made’, imekuwa moja ya wiski pendwa zaidi hapa nchini.
  Katika ziara yake hiyo ya siku mbili nchini, Hendriksz atakutana na wapenzi wa wiski katika matukio mbalimbali maalumu ikiwemo chakula cha mchana katika hoteli ya Dar Es Salaam Serena ambayo itawapa wapenzi wa Glenmorangie nafasi ya kuonja aina mbalimbali za wiski kutoka Glenmorangie.
  Pia Hendriksz anatarajiwa kutoa mafunzo maalumu kwa baadhi ya wahudumu kutoka katika bar kubwa ambayo yatagusa sio tu katika uchanganyaji sahihi wa wiski za Glenmorangie bali pia historia fupi na aina tofauti za Glenmorangie.
  Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwapa wahudumu ujuzi utakaowawezesha kutoa huduma bora na ya kipekee kwa wateja wao wakati wakiburudika na Glenmorangie kwenye bar au hotel wanazozipendelea.
  Balozi huyo pia anatarajiwa kupita katika sehemu mbalimbali zinazouzwa Glenmorangie kujibu maswali kutoka kwa umma pamoja na kuwapa aina tofauti ya kinywaji hicho wale ambao hawajawahi kuonja kinywaji hicho.
  Lakini kikubwa zadi kinachosubiriwa katika ziara hii ni tukio litakalofanyika jumanne usiku katika hoteli ya Hyatt Regency ambapo Hendriksz atafanya sherehe maalumu ya kuonja na kulinganisha vinywaji vya Glenmorangie.
  Huku kukiwa na nafasi ishirini tu kwa nchi nzima kuhudhuria sherehe hiyo, uhitaji baina ya wapenzi wa Glenmorangie kuhudhuria umekuwa mkubwa sana. Uonjaji rasmi wa kinywaji cha Glenmorangie utajumuisha kuonja ladha iliyokomaa vema ya vichanganyishi vya Glenmorangie huku ukipitia katika ladha tofauti tofauti, harufu pamoja na vionjo mbalimbali vinayoikamilisha Glenmorangie ikifuatiwa na chakula cha jioni maalumu kinachoendana sambamba na Glenmorangie.
  Zoezi hili limebuniwa maalumu ili kuwafundisha wanywaji wa Glenmorangie namna ambavyo watafurahia zaidi kinywaji chao cha Glenmorangie.
  Ziara ya Hendriksz itamalizika jumatano asubuhi hapa nchini ambapo ataelekea Nairobi kwa mwendelezo wa ziara hiyo hapa Afrika Mashariki.

  ####
  Kwa maelezo zaidi kuhusu ziara ya balozi wa Glenmorangie tafadhali piga simu no: +255774637777 au tuma barua pepe kwenda: marketing@qway-international.com

  Glenmorangie ni nini?
  Glenmorangie ni, kwa urahisi kabisa, aina ya kinywaji (wiski) yenye ladha nzuri na tamu kuliko yoyote ulimwenguni.
  Harufu yake nzuri na ladha ya kipekee huchangamsha akili na kuifanya uifurahie wakati wa kuinywa.
  Ikiwa na mchanganyiko wa kipekee zaidi ambao unaifanya kuwa kinywaji (wiski) itakayokuachia kumbukumbu ya pekee katika ladha, mchanganyiko na harufu nzuri.

  Kuhusu kampuni ya Glenmorangie
  Kampuni ya Glenmorangie ni mojawapo ya kampuni mashuhuri katika ubunifu na uuzaji wa bidhaa za wiski duniani kote na ni sehemu ya Moët Hennessy, kitengo cha mvinyo na pombe kali cha Moët Hennessy Louis Vuitton (LVMH).
  Makao yake makuu yako Edinburgh, Scotland, na Kampuni ya Glenmorangie pia inazalisha Glenmorangie Single Highland malt whiskey na Ardbeg Single Islay malt. Pia ndio wamiliki wa Scotch Whisky Malt Society.

  Wajibu wa mnywaji
  Kampuni ya Glenmorangie inasimamia unywaji makini na inashauri wanywaji wa Glenmorangie na Ardbeg whiskeys kunywa kwa kiasi na kwa kuzingatia miongozo iliyopendekezwa ya kiasi cha pombe kwa siku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BALOZI WA GLENMORANGIE AWASILI DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top