• HABARI MPYA

  Friday, October 26, 2012

  ARSENAL WAPATA MKATABA MPYA NA ADIDAS, WAITOSA NIKE

  New deal: Arsenal have been sponsored by Nike since 1994
  Arsenal imekuwa ikidhaminiwa na Nike tangu 1994

  Three stripes: Arsenal are poised to renew their association with Adidas
  Nembo tatu; Arsenal inajiandaa kuingia mkataba na Adidas


  KLABU ya Arsenal inaelekea kumaliza ushirikiano wake wa miaka 18 na kampuni ya Nike na kusaini mkataba mpya wa pauni Milioni 25 na wapinzani wa kampuni hiyo ya vifaa vya michezo, Adidas. 
  The Gunners imekuwa ikidhaminiwa na kampuni hiyo ya Marekani, Nike tangu mwaka 1994, lakini Adidas, ambao ni wadhamini wa wapinzani wao, Chelsea, wanajiandaa kuichukua klabu hiyo. 
  Kwa mujibu wa The Daily Telegraph, nembo hiyo ya Ujerumani itafufua uhusiano wake na Arsenal wakati klabu hiyo ya London itakapomaliza mkataba na Nike mwaka 2014.
  The Daily Telegraph limeripoti kwamba Fulham, inayodhaminiwa na Kappa, itaungana na Adidas pia, katika mpango wa kampuni hiyo ambao unachukuliwa kama wa kuliteka Jiji la London kisoka.
  Mbali na Manchester United na Barcelona, Arsenal ni klabu kubwa inayouza jezi za Nike kwa mashabiki wasiopungua 800,000 kila mwaka.   
  Mkataba wa Arsenal na Adidas utawafanya wapokee mara mbili ya fedha walizokuwa wakipewa na Nike, pauni Milioni 13 kwa msimu.

   Wanaouza jezi za klabu za Ligi Kuu England

  Arsenal - Nike (Marekani)
  Aston Villa - Macron (Italia
  Chelsea - Adidas (Ujerumani)
  Everton - Nike (American)
  Fulham - Kappa (Italia)
  Liverpool - Warrior (Marekani)
  Man City - Umbro (Uingereza
  Man United - Nike (Marekani)
  Newcastle - Puma (Ujerumani
  Norwich - Errea (Italia
  QPR - Lotto (Italia)
  Reading - Puma (Italia)
  Southampton - Umbro (Uingereza)
  Stoke - Adidas (Ujerumani)
  Sunderland - Adidas (Ujerumani)
  Swansea - Adidas (Ujerumani)
  Tottenham - Chini ya Armour 
  West Brom - Adidas (Ujerumani)
  West Ham - Macron (Italia)
  Wigan - Mi FIt (Uingereza)

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: ARSENAL WAPATA MKATABA MPYA NA ADIDAS, WAITOSA NIKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top