• HABARI MPYA

    Monday, October 29, 2012

    TENGA ACHEMSHA VITA YA RUSHWA TFF

    Rais wa TFF, Leodegar Tenga (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo, makao makuu ya shirikisho hilo, Ilala, Dar es Salaam. Kulia ni Sunday Kayuni, Mkurugenzi wa Ufundi na kushoto ni Angetile Osiah, Katibu Mkuu


    Na Mahmoud Zubeiry
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga amesema kwamba vita dhidi ya rushwa katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ni ngumu na inahitaji sapoti kubwa ya wadau na wapenzi wa mchezo wenyewe ili kuifanikisha.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, makao makuu ya TFF, Ilala mjini Dar es Salaam, Tenga alisema kwamba pamoja awali kuwepo kwa mazingira ya ushahidi wa rushwa, lakini wanashindwa kwa sababu wao wana mipaka yao.
    “Hili la rushwa kwa kweli ni gumu, ni gumu kwa sababu sisi tuna mipaka yetu, lazima tupate ushirikiano na vyombo husika. Lazima tupate ushirikiano wa wapenzi wenyewe wa mpira,”alisema Tenga.
    Beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, alisema wakati mwingine inakuwa vita hiyo inakuwa ngumu zaidi anaposikia hata Waandishi wa Habari wanahusika.
    “Mimi sijathibitisha, lakini watu wananiambia viongozi wenyewe wanashiriki mchezo huu. Tena nasikia hadi nyinyi Waandishi wa Habari wakati mwingine mnatumiwa kupenyeza rushwa, kwa kweli inasikitisha,”alisema Tenga.
    Kuhusu vipimo vya dawa za kulevya katika Ligi Kuu, Tenga alisema kwamba mchakato wa zoezi hilo unaendelea na walichokifanya kwa sasa ni kuwataaribu na kuwapa muda wahusika waache taratibu.
    Alisema wamewapa nusu msimu watumiaji wa mihadarati katika soka ya Tanzania kujiondoa taratibu na tayari wamekwishawaambia hadi  viongozi wa klabu zote, ili zoezi hilo likianza liende vizuri.
    “Hatutaki kuwaadhiri vijana wetu, ndiyo maana tumewaambia mapema, ili wale ambao wanavuta bangi kwa mfano, waanze taratibu kula chwingamu waache bangi, ili wakati utakapofika, hakutokuwa na mzaha,”alisema Tenga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: TENGA ACHEMSHA VITA YA RUSHWA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top