• HABARI MPYA

  Sunday, October 28, 2012

  MAMA CHIKU KUFUNGUA TAIFA CUP KIKAPU TANGA KESHO

  Mama Chiku Gallawa

  Na Mashaka Mhando, Tanga
  MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mama Chiku Gallawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa michuano ya Kombe la Taifa ya mpira wa Kikapu, Taifa Cup mwaka 2012 yanayotarajiwa kuanza kesho kwenye viwanja vya Mkwakwani na Harbours Club vilivyo jijini Tanga.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Tanga (TRBA), Hamisi Jaffary alisema maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri na waamuzi kumi na mbili ambao watachezesha mashindano hayo tayari wameshawasili jijini hapa tokea mwishoni mwa wiki.
  Jaffary alisema mashindano hayo yataanza Octoba 29 na kufikia tamati Novemba 5 mwaka huu na kushirikisha  mikoa mbalimbali hapa nchini ambapo mpaka juzi mikoa kumi na sita ilikwisha kuthibitisha kushiriki mashindano hayo.
  Mwenyekiti huyo aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Dar ,Arusha,Moshi,Iringa, Mbeya,Mara, Lindi,Shinyanga,Tabora,Dodoma  na Tanga ambao ndio wenyeji wa mashindano hayo ambapo alisema timu nyengine huenda zitathibitisha katika shirikisho la mipira wa kikapu Taifa ikiwemo Zanzibar ,Unguja na Pemba.
  Alisema mkoa  wa Kigoma walijitoa dakika za mwishoni kushiriki mashindano hayo ambayo msimu huu idadi ya washiriki imeongezeka kutokana na kuongezwa kwa idadi ya mikoa.
  Mashindano hayo wa mara ya kwanza yalifanyika jijini Tanga 1989 na mara ya mwisho ili kuwa ni 2005 msimu huu shamra shamra zimeonekana kuwa ni muda kubwa kutokana na kuwa maandalizi ya maandalizi yanayofanywa na mikoa shiriki huku viwanja ambazo zitatumika mashindano zimefanyiwa ukarabati wa hali ya juu.
  Mkoa wa Tanga unatarajiwa kuwa na wageni watapao 450 ikiwemo wachezaji na viongozi wa timu ambazo zitashiriki michuano hiyo na kutoa wito kwa wakazi wa Tanga kujitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hiyo.
  Aliongeza kuwa timu  zilianza  kuwasili jijini Tanga tokea Jumamosi na Jumapili ambapo kesho ndio ufunguzi rasmi wa mashindano hayo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MAMA CHIKU KUFUNGUA TAIFA CUP KIKAPU TANGA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top