DIDIER DROGBA KUREJEA ENGLAND KUKIPIGA LIVERPOOL 

Liverpool inataka kumchukua kwa mkopo mshambuliaji wa Shanghai Shenhua, Didier Drogba, mwenye umri wa miaka 34, mara Ligi Kuu ya China itakapomalizika wiki ijayo.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anataka kumsajili winga wa Newcastle United, Hatem Ben Arfa, mwenye umri wa miaka 25,baada ya kukubali kumpoteza Theo Walcott Januari.
Mario Balotelli, mwenye umri wa miaka 22, anatakiwa na AC Milan na klabu hiyo ya Italia iko tayari kuuza nyota wake kadhaa ili kumsajili mshambuliaji huyo wa Manchester City.

STEWART ROBSON ATOA USHAURI WA BURE ARSENAL UBUTU WA BEKI

Stewart Robson amesema kwamba matatizo ya safu ya ulinzi ya Arsenal yanaweza kumalizwa kwa ushirikiano wa pamoja nabaina ya Kocha Msaidizi na beki wa zamani wa kati wa Gunners, Steve Bould na Kocha Mkuu, Wenger.
Manchester United imemtambulisha Kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola kama mtu ambaye wanataka arithi mikoba ya Sir Alex Ferguson atakapoondoka Old Trafford.
Kocha wa St Johnstone, Steve Lomas, mwenye umri wa miaka 38, amesema kwamba hawezi kuzipuuza tetesi za yeye kuhusishwa na kuhamia Burnley.

MANCINI ATAKA KIKAO NA MWENYEKITI MAN CITY, OFISA MPYA MTENDAJI 

Kocha wa Manchester City, Roberto Mancini anataka kuzungumza na Mwenyekiti, Khaldoon Al Mubarak na Ofisa mpya Mtendaji Mkuu, Ferran Soriano ili kujua kama watarusiah sapoti yao kamili kwake, katika kutafuta namna ya kumrudhishia mamlaka ya kwenye chumba cha kubadilishia nguo.