• HABARI MPYA

  Sunday, October 21, 2012

  CHEKA KUZIPIGA NA MJERUMANI NOVEMBA 18 KUWANIA TAJI LA IBF


  Francis Cheka
  Na Prince Akbar
  BONDIA Francis Cheka ‘SMG’ anatarajiwa kupanda ulingoni kuzipiga na Benjamin Simon wa Ujerumani Novemba 18, mwaka huu kwenye ukumbi wa Universal, mjini Berlin nchini Ujerumani.
  Awali mpambano huo ulikuwa ufanyike Novemba 17 mjini humo, lakini umesogezwa mbele kwa siku moja na tayari Cheka amemwishashasaini mkataba wa kukutana na mbabe huyo wa Ujerumani anayejulikana kwa jina la utani, Iron Ben kutokana na ukali wa makonde yake.
  Benjamin Simon
  Benjamin Simon amepigana mara 24 na kupoteza pambano moja tu, wakati Cheka katika mapambano yake 33 amepoteza sita.
  Katika barua aliyomuandikia Eva Rolle wa kampuni ya Prime Time Event Management ya Ujerumani, inayoandaa pambano hilo, Mwenyekiti wa IBF/USBA, Lindsey Tucker alimfahamisha kuwa Rais wa IBF/USBA Daryl Peoples au yeye mwenyewe, Lindsey Tucker watawasiliana na mama huyo kuhusu maofisa watakaosimamia mpambano huo.
  Hili litakuwa pambano la kwanza baina ya wababe hao, wakiwaniataji la IBF la Mabara (IBF Inter Cintintal) na mpambano wao unategemnea kutoa ushindani mkubwa.
  Mshindi katika mpambano huo ataingia moja kwa moja katika orodha ya mabondia 15 bora kwenye uzito wa Super Middle duniani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: CHEKA KUZIPIGA NA MJERUMANI NOVEMBA 18 KUWANIA TAJI LA IBF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top