• HABARI MPYA

  Thursday, October 25, 2012

  KIPIGO CHA REAL MADRID CHAIWEKA MGUU NJE MAN CITY ULAYA

  MATUMAINI ya Manchester City kufuzu hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yamepungua baada ya Borussia Dortmund kuifunga mabao 2-1 Real Madrid nchini Ujerumani. 
  Matokeo hayob yanaipeleka Dortmund kileleni mwa kundi mbele ya timu ya Jose Mourinho, wakati City wanashika mkia wakiwa na pointi moja tu baada ya kucheza mechi tatu.
  Robert Lewandowski alifunga bao dakika ya 36, kabla ya Cristiano Ronaldo kusawazisha ndani ya dakika mbili, lakini Marcel Schmelzer akawafungia wenyeji la ushindi dakika ya 64.
  Party time: Borussia Dortmund celebrate beating Real Madrid
  Borussia Dortmund wakishangilia kuifunga Real Madrid
  Winner: Marcel Schmelzer slams home Dormund's second goal
  Marcel Schmelzer akiifungia bao la ushindi Dormund

  Olympiacos walipata ushindi wa kwanza wakitoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Montpellier nchini Ufaransa na kuongeza ugumu katika Kundi B, baada ya Arsenal kufungwa na Schalke.
  Gaetan Charbonnier aliifungia Montpellier dakika ya 49kabla ya Vassilas Torosidis kusawazisha dakika ya 73 na Kostas Mitroglou aliyetokea benchi akafunga la ushindi dakika za majeruhi.
  Matokeo ya jana yanaipeleka Schalke kileleni kwa pointi zake saba, wakiizidi moja The Gunners, na Olympiacos inakwenda nafasi ya tatu na Montpellier inaburuza mkia.
  Big win: Olympiakos boosted their chances of qualifying
  Olympiakos wamejiweka katika nafasi nzuri

  Malaga imeendeleza wimbi la ushindi kileleni mwa Kundi C baada ya kuifunga AC Milan 1-0 na sasa inaongoza kundi hilo kwa pointi tatu zaidi. Joaquin ndiye aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 64 kwa pasi ya Manuel Iturra.
  Mechi nyingine ya Kundi C, Zenit St Petersburg waliifunga 1-0 Anderlecht nchini Urusi. 
  Alexander Kerzhakov alifunga dakika ya 72 kwa mkwaju wa penalti, baada ya Milan Jovanovic kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari na Alexander Anyukov.
  Katika Kundi A, Porto imeendeleza rekodi yake nzuri ya asilimia 100 kwa ushindi wa 3-2 dhidi ya Dynamo Kiev nchini Ureno.
  Wageni walisawazisha mara mbili kupitia kwa Oleg Gusev na Ideye Brown baada ya wenyeji kufunga kupitia kwa Silvestre Varela na Jackson Martinez, kabla ya Martinez kufunga la ushindi zikiwa zimesalia dakika 12.
  Despair: AC Milan were beaten by Spanish side Malaga
  AC Milan walifungwa na Malaga ya Hispania

  Katika Kundi A, Paris St Germain ilikwea nafasi ya pili kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dinamo Zagreb nchini Croatia, Zlatan Ibrahimovic akifunga la kwanza dakika ya 32 na Jeremy Menez akafunga la pili kabla ya mapumziko.

  SOURCE: http://www.dailymail.co.uk
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: KIPIGO CHA REAL MADRID CHAIWEKA MGUU NJE MAN CITY ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top