• HABARI MPYA

  Saturday, October 27, 2012

  AZAM AKADEMI WAICHAPA SIMBA B

  Azam B imeifunga Simba B 1-0, bao pekee la Kevin Friday dakika ya 56 katika mchezo wa utangulizi kabla ya mechi za timu za wakubwa za klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.  Pichani wachezaji wa Azam B, maarufu kama Azam Academy wakishangilia bao lao pekee la ushindi kwa kumpongeza mfungaji, Kevin kulia. Tazama picha zaidi za mechi hiyo.

  Kocha wa makipa wa Simba, James Kisaka akishuhudia mechi hiyo

  Makocha Waserbia, Boris Bunjak wa Azam kushoto na Milovan Cirkovick wa Simba kulia wakijadiliana huku wakiangalia mechi hiyo  

  Mgaya Abdul wa Azam akikokota mpira, dhidi ya Miraj Athumani wa Simba. Kulia ni Abdallah Seseme aliyeipa mgongo kamera

  Mgaya Abdul akipiga mpira mbele ya Omary wa Simba

  Jamil Mchauro wa Azam akitoa pasi kwa Mange Chagula mbele ya Kemmy Ally wa Simba

  Vijana wakionyeshana ufundi

  Kocha Mkuu wa Azam Academy, Vivek Nagul akiwa na Msaidizi wake, Philipo Alando

  Vijana wakionyesha ufundi

  Mmoja wa |Maofisa wa benchi la Ufundi la Azam, Jemedari Said Kazumari

  MIraj Athumani wa Simba akikosa bao la wazi

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: AZAM AKADEMI WAICHAPA SIMBA B Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top