• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 26, 2012

  PIGO MAN UNITED, KAGAWA NJE MWEZI MZIMA


  KIUNGO wa Manchester United, Shinji Kagawa anakabiliwa na maumivu ya goti, ambayo yatamuweka nje ya Uwanja kwa wiki tatu hadi nne.
  Kocha wa United, Sir Alex Ferguson amethibitisha habari hizo katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo.
  "Kagawa atakuwa nje kwa wiki tatu hadi nne kutokana na maumivu ya goti. Aliumia katika mechi na Braga Jumanne katika Ligi ya Mabingwa,"alisema Mscotland huyo.
  Shinji Kagawa of Manchester United feels the pain of an injury
  Shinji Kagawa of Manchester United feels the pain of an injury
  Shinji Kagawa akisikilizia maumivu katika mechi na Braga
  Missing man: Sir Alex Ferguson is disappointed to have lost a star man
  Sir Alex Ferguson amesononeshwa na kuumia kwa nyota wake huyo
  Katika hatua nyingine, Ferguson amesema beki Chris Smalling amerejea mazoezini baada ya kupona.
  "Hiyo ni zawadi kubwa kwetu, Phil Jones anaanza mazoezi pia," alisema kuhusu Jones, aliyeumia goti mwezi uliopita mazoezini.
  Jumping for joy: Chris Smalling is back in the fold after a lengthy lay off
  Chris Smalling aliyeruka juu, amerudi kazini
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: PIGO MAN UNITED, KAGAWA NJE MWEZI MZIMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top