DE GEA AIKATAA REAL MADRID AKISEMA ANAFURAHIA MAISHA MAN UNITED

MALOUDA KARIBU KABISA NA MLANGO WA KUTOKEA CHELSEA

Florent Malouda anatumai kumaliza maisha yake Chelsea, baada ya klabu ya Santos kuanza harakati za kumsajili winga huyo wa Kifaransa mwenye umri wa miaka 32.
Kipa David de Gea, mwenye umri wa miaka 21, amesema anafurahia maisha Manchester United na hatarajii kurejea Hispania, licha ya taarifa kwamba Real Madrid wanamtaka.
Chelsea, Manchester United na Liverpool zote zilimfuatilia beki wa pembeni wa Genoa, Mario Sampirisi, mwenye umri wa miaka 19, timu yake ikicheza na AC Milan Jumamosi.
Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson inataka kumsajili beki wa kimataifa wa Uruguay anayechezea klabu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa, Diego Lugano, mwenye umri wa miaka 31.

MARK HUGHES KATIKA WIKI NGUMU

Kocha wa Queens Park Rangers, Mark Hughes anakabiliwa na wiki ngumu na anaweza kufukuzwa kazi iwapo hatashinda mechi yake ya wiki ijayo dhidi ya Reading.
Kocha wa West Ham, Sam Allardyce amesema mshambuliaji Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 23, bado anahitaji ulinzi zaidi kutoka kwa marefa.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amemtaka Roy Hodgson kutomchukua Jack Wilshere, mwenye umri wa miaka 20, katika mchezo wa kirafiki wa England dhidi ya Sweden mwezi ujao.