• HABARI MPYA

  Tuesday, October 23, 2012

  MECHI YA MTIBWA NA JKT RUVU YASOGEZWA MBELE

  MECHI namba 79 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Mtibwa Sugar na JKT Ruvu (pichani) iliyopangwa kuchezwa Novemba 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro, imesogezwa mbele hadi Novemba 7, mwaka huu.
  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba mabadiliko hayo yamefanyika kwa vile Novemba 4 mwaka huu, Mtibwa Sugar itacheza mechi namba 30 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro.
  Wambura alisema kwamba, mechi hiyo awali ilikuwa ichezwe Oktoba 3, mwaka huu lakini ikabadilishwa ili kutoa fursa kwa mechi za Super Week zilizoonyeshwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha Super Sport cha Afrika Kusini.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MECHI YA MTIBWA NA JKT RUVU YASOGEZWA MBELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top