JUVENTUS YAPANGA KUIFANYIA KITU MBAYA ARSENAL, WENGER AMPATA MRITHI WA WALCOTT

Juventus inajiandaa kuipiga bao Arsenal katika mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa Atletico Madrid, Fernando Llorente, mwenye umri wa miaka 27, na kisha ijaribu kumsajili mshambuliaji wa Washika Bunduki hao, Theo Walcott, mwenye umri wa miaka 23.
Florent Malouda
Florent Malouda  
Kiungo wa Chelsea, Florent Malouda, mwenye umri wa miaka 32, anaweza kuhamia Santos ya Brazil ifikapo Januari mwakani.
Manchester United imeambiwa na wakala wa mchezaji wanaweza kufanya mpango wa kumsajili kiungo wa PSV Eindhoven, Kevin Strootman, mwenye umri wa miaka 22 mwishoni mwa msimu.
West Brom inajipanga kwa usajili wa maana mwishoni mwa msimu, kwa mujibu wa Mkurugenzi wao wa Ufundi, Dan Ashworth.
Birmingham City inafanya mazungumzo na klabu nyenzake ya Daraja la Kwanza, Blackpool ili kumchukua kwa mkopo kiungo, Barry Ferguson, mwenye umri wa miaka 34.

HUYU NDIYE MRITHI WA WALCOTT ARSENAL

Arsenal inapanga kumpandisha winga Serge Gnabry, mwenye umri wa miaka 17, katika kikosi chake cha kwanza iwapo Theo Walcott, mwenye umri wa miaka 23, ataondoka kwenye klabu hiyo Januari.