• HABARI MPYA

  Friday, February 24, 2012

  'SIMBA NA YANGA' UWANJANI KAMPALA KESHO

  LIGI Kuu ya Uganda, maarufu kama Bell Super League moto wake utawaka kuanzia jioni ya leo, lakini mpango mzima ni kesho wakati Simba na Yanga za huko, SC Villa ‘Jogoo’ na Express FC ‘Tai Mwekundu’ zitakapoumana. Express vs SC Villa unamaanisha mpambano wa wapinzani wa jadi Uganda ambao una mvuto wa aina yake.
  Mabingwa mara sita – Express – wanashika nafasi ya pili kwa pointi zao 30 na Villa wapo nafasi ya tisa kwa pointi zao 23. Jogoo pia limecheza mechi mbili zaidi ya Tai Mwekundu, 15.
  Timu hizo mbili zilipokutana mara ya mwisho katika mzunguko wa kwanza wa Ligi kwenye Uwanja wa Namboole, Oktoba, Express ilishinda mabao 2-0, Bonny Baingana akifunga bao tamu kupita maelezo, tena kwa jitihada zake binafsi.
  Hiyo ilikuwa mechi ya kwanza Villa inacheza tangu kocha wake Mserbia, Srdjan Zivojnov aliyewahi kuinoa Yanga atupiwe virago.
  Lakini kesho, Tai Mwekundu watamkosa Baingana – mshambuliaji aliyesafiri kwenda Rwanda kujiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Uganda chini ya miaka 20 wiki ijayo.

  RATIBA KAMILI LIGI YA UGANDA KUANZIA LEO:
  leo, February 24, saa 10.30 jioni
  Fire Masters vs URA, Kavumba
  Masaka vs Proline, Masaka, saa 10.00 jioni
  KCC vs Simba, Nakivubo
  Bunnamwaya vs Bidco, Buikwe, saa 10.00 jioni
  Police vs Utoda, Namboole,
  Kesho, February 25, saa 9:00 alasiri
  Water vs Maroons, Luzira
  Express vs SC Villa –Wankulukuku
  Victors vs Hoima-Busia, Kakindu
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: 'SIMBA NA YANGA' UWANJANI KAMPALA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top