• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 29, 2012

  TBL YADHAMINI MEDIA DAY BONANZA


  WAKATI tamasha maalum kwa vyombo vya habari ‘Media Day’  kwa mwaka 2012 likipangwa kufanyika Machi 24 kwenye ufukwe wa Msasani, Kampuni ya  bia Tanzania (TBL) imetoa shilingi mil.62.5 kwa ajiliya kudhamini tamasha hilo.
   Mkurugenzi wa Uhusiano wa Jamii na Sheria wa TBL Steven Kilindo alisema kuwa wameamua kudhamini tamasha hilo kutokana na kuthamini mchango wa waandishi wa habari katika biashara za kampuni yao.
  “TBL itahakikisha bonanza la mwaka huu linafana na litakuwa la aina yake kuanzia katika michezo, burudani, vinywaji na vyakula, hivyo tunawaomba waandishi wajitokeze kwa wingi ili kuweza kubiridika pamoja na kubadilishana mawazi,”Alisema Kilindo.
  Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) ambayo ndiyo waandaaji wa bonanza hilo Juma Pinto, pamoja na kuishukuru TBL kwa udhamini huo aliiomba kutoishia kudhamini kwenye mabonanza tu bali wafanye hivyo hata katika mafunzo mbalimbali yanayoaandaliwa na chama hicho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TBL YADHAMINI MEDIA DAY BONANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top