• HABARI MPYA

  Tuesday, February 21, 2012

  REAL MADRID YATOKA SARE YA CSKA

  MCHEZAJI Pontus Wernbloom alifunga katika dakika ya tatu ya muda wa nyongeza na kuiwezesha timu yake CSKA Moscow kupata sare ya 1-1 na Real Madrid katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu. Wernbloom alikutana na mpira ambao ulimbabatiza beki wa Madrid, Alvaro Arbeloa na kuusukuma nyavuni.
  Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Luzhniki mjini Moscow, Urusi, Mreno Cristiano Ronaldo aliifungia Real Madrid bao la kuongoza dakika ya 28, hilo likiwa bao lake la 36 msimu huu.
  Mechi ya marudiano baina ya timu hizo itapigwa Hispania Machi 14, mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YATOKA SARE YA CSKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top