• HABARI MPYA

  Saturday, February 25, 2012

  CHELSEA YAREJEA TOP FOUR ENGLAND, TORRES BADO KITUKO

  LONDON, England KLABU ya Chelsea jana iliibuka na ushindi waq mabao 3-0 dhidi ya Bolton na kufanikiwa kurejea ndani ‘top four’ kwenye Ligi Kuun ya England sambamba na kumpunguzia jakamoyo kocha wake, Andre Villas-Boas.
  Shukrani kwao David Luiz, Didier Drogba na Frank Lampard kwa mabao yao ya kipindi cha pili yaliyozimja gundu la Chelsea kucheza mechi tano bila kushinda, hali ambayo ilikuwa inakiweka matatani kibarua cha kocha Villas-Boas.
  Ushindi huo unaifanya klabu hiyo ya London ipande nafasi ya nne, juu ya Arsenal.
  Bolton wanabaki kwenye ‘maeneo’ ya kushuka na wameshindwa kuvunja mwiko wa kutoifunga Chelsea tangu mwaka 2003. Torres aliingia kuchukua nafasi ya Drgoba kipindi cha pili, lakini hakufunga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAREJEA TOP FOUR ENGLAND, TORRES BADO KITUKO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top