• HABARI MPYA

    Wednesday, February 29, 2012

    El Saadat kushuka na madude toka Uholanzi Jumaosi


    RAIS wa bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ Nyoshi El Saadat anatarajiwa kurejea nchini Ijumaa  akitokea nchini Uholanzi alipokwenda kuzifanyia  ‘Mastering’ nyimbo zao nne ambazo zitakuwemo kwenye albamu yao mpya zitakazokuwemo kwenye albamu yao mpya inayokwenda kwa jina la 'Chuki ya Nini' na kuzitaja nyimbo hizo ni pamoja na  Otilia, Ndoa ya Kisasa, Dai Chako Ulaumiwe na Fataki.
      Mara baada ya kuwasili siku hiyo atahudhuria onyesho la bendi hiyo litakalofanyika kwenye ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho, uliopo Kijitonyama jijini dar es Salaam  ambalo litakuwa mahususi kwa ajili ya kumkaribisha.
     “Nawaomba mashabiki wa FM Academia mjitokeze kwa wingi siku hiyo katika ukumbi wetu pale Makumbusho kwani pamoja na burudani toka kwa bendi yenu pia nitakuja na mazawadi kutoka Uholanzi ambayo yote ni sehemu ya kuwapa raha,”Alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: El Saadat kushuka na madude toka Uholanzi Jumaosi Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top