• HABARI MPYA

  Monday, February 20, 2012

  PSG CHUPUCHUPU KULIZWA NA UTAKA UFARANSA

  TIMU ya Paris Saint-Germain ilihitaji bao la kusawazisha ili kupata sare ya 2-2 dhidi ya Montpellier na kuwazidi kwa pointi moja wapinzani wao.
  Uwezo binafsi wa Jeremy Menez wa kuuchezea mpira uliwasaidia PSG kuchomoa dakika ya 88, baada ya winga kumnyanyasa beki wa Montpellier, Mapou Yanga-Mbiwa na kumtengenezea Guillaume Hoarau nafasi ya kufunga.
  Beki wa kati wa PSG, Alex alifunga bao la kuongoza kwa shuti la umbali wa mita 30 dakika ya 41, lakini Younes Belhanda akasawazisha kwa kichwa dakika ya 45.
  Mshambuliaji wa Nigeria, John Utaka aliifungia Montpellier bao la kuongoza akimalizia krosi ya Olivier Giroud dakika ya 82.
  Katika mechi nyingine jana, Lyon iliifunga 1-0 Bordeaux, Saint-Etienne iliitandika Rennes 4-0 na kupanda hadi nafasi ya sita ikilingana kwa pointi na Marseille, Lyon na Rennes.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PSG CHUPUCHUPU KULIZWA NA UTAKA UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top