• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 20, 2012

  HUNTELAAR AING'ARISHA SCHALKE BUNDESLIGA

  MSHAMBULIAJI Klaas-Jan Huntelaar alifunga mabao mawili na kuisaidia Schalke kuilaza Wolfsburg mabao 4-0 katika Bundesliga jana. Huntelaar pia alipiga penalti iliyookolewa na kipa wa Wolfsburg, Diego Benaglio. Huntelaar sasa analingana na Mario Gomez wa Bayern Munich kwa mabao, kila mmoja 18 na Schalke inaongoza Bundesliga kwa jumla ya mabao 50.
  Hannover iliifunga Stuttgart 4-2, Christian Pander akifunga moja na kupika mawili.
  Borussia Dortmund inaongoza ligi hiyo ikiizidi pointi tatu Borussia Moenchengladbach.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HUNTELAAR AING'ARISHA SCHALKE BUNDESLIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top