• HABARI MPYA

  Sunday, February 19, 2012

  MCHAKATO WA MABONDIA WA OLIMPIKI YA LONDON 2012 WAZIDI KUNOGA

  MABONDIA 17 wamechaguliwa kuendelea kubakia katika kambi ya timu ya taifa ya ndondi za Ridhaa, katika mchakato wa kutafuta timu ya kushiriki michuano ya Olimpiki, itakayofanyika London mwaka huu. Mabondia walioteuliwa kutokana na mashindano ya mchujo yaliyomalizika Ijumaa ni John Christian na Said Pume uzito was Light Fly, Abdallah Kassim na George Constantine uzito wa Fly, Emillian Patrick na Undule Langson uzito wa Bantam, Dennis Martine na Fabian Gaudence uzito wa Light.
  Wengine ni Victor Njaiti na Hamisi Kitenge uzito wa Light Welter, Mohamed Mhibumbui uzito wa Welter, Suleiman Kidunda uzito wa Middle, Abdul Rashid uzito wa Light Heavy, Mhina Morris na Haruna Swanga, Nuru Ibrahim uzito wa Heavy na Maxmillian Patrick uzito wa Super Heavy.
  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT), Makore Mashaga alisema kwamba mabondia wote wanatakiwa kuripoti ofisi za BFT keshokutwa, ili wapewe utaratibu wa kuanza mazoezi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MCHAKATO WA MABONDIA WA OLIMPIKI YA LONDON 2012 WAZIDI KUNOGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top