• HABARI MPYA

  Tuesday, February 21, 2012

  TABORA MARATHON YAJA

  CHAMA cha riadha mkoa wa Tabora,(RITAM),kwa kushirikiana na Orion Tabora Hotel,wanatarajia kuendesha mashindano yatakayojulikana kama Tabora Marathon 2012 kwa lengo la kuutangaza mkoa na vivutio vyake.
  Mratibu wa mashindano hayo,Ramadhan Makula,akizungumza na waandishi wa habari,katika Orion Hotel,alisema lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji,kutangaza vivutio vilivyoko Tabora na kuaandaa vijana katika medani ya kitaifa na kimataifa.
  Makula alisema wadhamni wa mashindano hayo ni Orion Tabora Hotel,chini ya usimamizi wa mkurugenzi wa hotel hiyo Poley Ahmed na mashindano hayo yanatarajia kushirikisha watu 400 wa rika mbalimbali.
  Alisema licha kuasisis mashindano hayo ambayo yatakuwepo kila mwaka,Makula alisema kutakuwa na kazi za kuboresha maeneo ya kihistoria mkoani hapa ambayo ni Living stone Museum iliyopo Kwihara kata ya Itetemia manispaa Tabora.
  Aliongeza maeneo hayo yataboreshwa kwa kupaka rangi hali ambayo itawawezesha wananchi na wageni mbalimbali kupata fursa ya kutembelea maeneo hayo ambayo yako kwenye historia ya nchi.
  Maratibu huyo alisema wmeamua kufanya hivyo kwa kuwa wana uzalendo mkubwa na mkoa wa Tabora kwani bado mkoa haupewi kipaumbele licha ya kuwa ni mkoa wenye uiwingi wa mambo ya utalii na hata kisiasa.
  Naye mdhamini mkuu wa mashindano hayo na mkurugenzi wa Orion Tabora Hotel,Poley Ahmed alisema na kutoa wito kwa vijana wa mkoa wa Tabora kujitokeza kwa wingi kushirikia mashindano hayo ambayo yatakuwa na zawadi mbalimbali katika kilele chake.
  Alisema licha ya yeye kuwa madhamni pia ameomba na wadau wa mchezo huo na wafadhili mbalimbali kujitokeza kufadhili mashindano hayo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TABORA MARATHON YAJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top