• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 24, 2012

  STARS, DRC YAINGIZA KIASI CHA MBOGA, ILA MAKATO YAKE SASA UTAKOMA NAYO!

  Pambano la kirafiki la kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC (Leopards) lililofanyika jana (Februari 23 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 32,229,000.
  Fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 11,420 waliokata tiketi kushuhudia mechi kwa kiingilio cha sh. 2,000, sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000 na sh. 15,000.
  Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 5,916,288, gharama ya kuchapa tiketi sh. 2,250,000, malipo kwa kamishna wa mchezo sh. 150,000, malipo kwa waamuzi wanne sh. 480,000, ulinzi na usafi kwa Uwanja wa Taifa sh. 2,350,000, Wachina sh. 2,000,000, umeme sh. 300,000 na maandalizi ya uwanja (pitch marking) sh. 400,000.
  Nyingine ni asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 3,676,542, asilimia 10 ya uwanja sh. 1,838,271, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 919,136 na asilimia 65 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 11,948,763.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STARS, DRC YAINGIZA KIASI CHA MBOGA, ILA MAKATO YAKE SASA UTAKOMA NAYO! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top