• HABARI MPYA

  Monday, February 20, 2012

  CHELSEA YABEBA MATUMAINI YA ENGLAND ULAYA, INA KIBARUA NA NAPOLI KESHO

  TIMU ambayo imeshuka kimchezo na morali, Chelsea inajiandaa kwa mchezo mgumu wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Napoli kesho, ikiwa ndio inabeba hatima ya klabu za England kwenye michuano hiyo.
  Huku Manchester United na Manchester City zikiwa zimekwishatolewa na kuanguki Europa League na Arsenal inachungulia mlango wa kutokea, Chelsea ndiyo pekee inayotazamwa kwa sasa kama inaweza kutinga Robo Fainali.
  Ikumbukwe England imeingiza timu sita fainali katika fainali 12 za Ligi ya Mabingwa zilizopita.
  Chelsea ina rekodi nzurim, ikiwa imecheza Nusu Fainali nne na kutinga fainali ya mwajka 2008, lakini imeporomoka hadi nafasi ya tano katika Ligi Kuu na iliambulia sare ya1-1 na Birminghma kwenye Kombe la FA Jumamosi.
  Wakati kocha wa Chelsea Andre Villas-Boas wiki iliyopitaa aliangushwa na wachezaji wake, Napoli iko ‘full’ na inajiamini hasa kutokana na ushindi wa mabao 3-0 walioupata dhidi ya Fiorentina Ijumaa.
  Edinson Cavani alitupia mawili na kufikisha mabao 15 kwenye Serie A.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YABEBA MATUMAINI YA ENGLAND ULAYA, INA KIBARUA NA NAPOLI KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top