• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 25, 2012

  MAN UNITED NAO WANA KAZI YAO KESHO

  KIKOSI cha Norwich City kina hofu ya majeruhi kama Kyle Naughton na Zak Whitbread, huku Daniel Ayala akiendelea kuwa nje kutokana na maumivu ya nyama za paja. Marc Tierney ndiye anatarajiwa kuwemo kwenye kikosi hicho.
  Hivyo kocha Paul Lambert atalazimika kuwachezesha Russell Martin na Elliott Ward, ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika mechi zilizopita.
  Jed Steer alianza katika mchezo wa Kombe la dhidi ya timu ya Leicester na kufungwa mabao 2-1, lakini John Ruddy yuko tayari kurejea kama ilivyo kwa Grant Holt, ambaye amekosa mechi ya raundi ya tano walipokutana kwa mara ya mwisho na Manchester United.
  Sir Alex Ferguson aliwapumzisha wachezaji wake  kwenye mchezo wa pili Ligi ya Europa dhidi ya Ajax, na kuwapumzisha akina Rio Ferdinand, Michael Carrick, Paul Scholes, Patrice Evra na Jonny Evans kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England ili kuendelea kwuafukizia wapinzani wao Manchester City.
  Wayne Rooney alikosa mchezo wa wa Ligi hiyo ya Europa kutoka na kuwa mgonjwa na maamuzi yatafanywa baadaye kama ataweza kucheza au la, Nani huenda akaanza.
  Hofu nyingine kwa United iko kwa Tom Cleverley, ambaye anasumbuliwa na kifundo cha mguu, naye Antonia Valencia ana maumivu ya nyama, akiwacha mlango wazi kwa Ryan Giggs kurejea baada ya kukaa benchi katikati ya wiki. Anderson, ambaye alifunga wakati timu hizo zilipokuta huenda akarejea.
  Norwich City: Ruddy, Naughton, R. Martin, Ward, Drury, Pilkington, Hoolahan, Fox, Surman, Holt, Morison.
  Manchester United: De Gea, Rafael, Ferdinand, Evans, Evra,Young, Scholes, Carrick, Giggs, Rooney, Welbeck.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED NAO WANA KAZI YAO KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top