John Bocco wa Azam na Hussein Javu wa Mtibwa Sugar, nchi inahitaji kuwekeza kwa wachezaji hawa ili wawe washambuliaji tegemeo wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Hawa watu wanahitaji kulishwa vitu vya zaida ambavyo wanakosa sambamba na elimu ya kujitambua, waache ulimbukeni wa kulewa sifa, wawe na malengo ya kufika mbali, ili wajibidiishe zaidi. Ni watu ambao wanaweza kazi na kama taifa litaamua kuwekeza kweli kwa watu hawa, tutakuwa na miaka mitatu ya kushangilia mabao yao. Watu wanaweza kuufanya mpira ukae kwenye eneo la wapinzani. Wana uwezo. Tuwape nafasi na tuwape muda kabla ya kuanza kula matunda yao.
Former England star James Haskell blunders into women's rugby row after 'have a day off' post
-
The former England back-rower told Bristol Bears star Simi Pam to 'have a
day off' when she corrected his social media post listing the most-capped
front-r...
Dakika 17 zilizopita
0 maoni:
Chapisha Maoni