Bondia Muingereza David Haye, katikati, akiwa na rafiki zake wakipita katika Uwanjua wa Ndege wa Heathrow, London kuelekea Marekani jana. Haye aligombana na bondia mwenzake wa Uingereza, Dereck Chisora aliyetoka kuzipiga na Vitali Klitschko, mjini Munich, Ujerumani Jumamosi. Bodi ya Ngumi Uingereza inafanya uchunguzi juu ya tukio hilo juu ya Chisora na ikibainika atachukuliwa hatua. Haye hawezi kuchukuliwa hatua, kwa sababu bondia huyo wa London amestaafu ndondi mwaka jana baada ya kupiwa na mdogo wake Klitschko, Wladimir, lakini inaaminika Haye anatafutwa na Polisi wa Ujerumani kwa mahojiano juu ya tukio hilo.
Thank God it is Monday: Pastor Hassan on his new book, embracing work early on
-
Dakika 22 zilizopita
0 maoni:
Chapisha Maoni