• HABARI MPYA

  Friday, February 24, 2012

  AC MILAN YAPATA PIGO SAA CHACHE KABLA YA KUIVAA JUVE

  KLABU ya AC Milan imepata pigo ikiwa inaelekea kwenye mchezo mgumu dhidi ya Juventus Serie A, baada ya mshambuliaji wake tegemeo, Zlatan Ibrahimovic kufungiwa.
  Msweden huyo tishio alitolewa kwa kadi nyekundi katika mechi dhidi ya Napoli, Februari 5 kwa kumpiga kibao Salvatore Aronica na kwa kosa hilo, amefungiwa mechi tatu.
  Milan imekata rufaa kumpigania mchezaji huyo afungiwe mechi mbili tu, adhabu ambayo itampa Ibrahimovic fursa ya kucheza dhidi ya Juve kesho.
  Sasa Milan italazimika kupigana bila mfungaji bora na mchezaji wake nyota katika mchezo huo mgumu wa msimu. Milan inaizidi Juve pointi moja ikiwa imecheza mechi moja zaidi.
  Pamoja na hayo, katika mechi zao mbili zilizopita, bila  Ibrahimovic hawakuonyesha kutetereka wakiifunga Udinese 2-1 na Cesena 3-1.

  RATIBA SERIE A:
  Februari 25, 2012
  Genoa v Parma (saa 2:00 usiku)
  AC Milan v Juventus (saa 4:45 usiku)
  Februari 26, 2012
  Chievo v Cesena (saa 11:00 jioni)
  Cagliari v Lecce (saa 11:00 jioni)
  Catania v Novara (saa 11:00 jioni)
  Siena v Palermo (saa 11:00 jioni)
  Atalanta v Roma (saa 11:00 jioni)
  Bologna v Udinese (saa 4:45 usiku)
  Lazio v Fiorentina (saa 4:45 usiku)
  Napoli v Inter Milan (saa 4:45 usiku)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AC MILAN YAPATA PIGO SAA CHACHE KABLA YA KUIVAA JUVE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top