• HABARI MPYA

  Monday, February 20, 2012

  DRC WAJA KWA MAFUNGU KUIVAA STARS

  KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Claude Le Roy na msaidizi wake wamewasili nchini juzi mchana kwa ndege ya Emirates wakitokea Paris, Ufaransa tayari kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Taifa Stars.
  Mechi hiyo itafanyika Februari 23 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mfaransa Le Roy ambaye alianza kuifundisha DRC mwezi Septemba mwaka jana na msaidizi wake wamefikia kwenye hoteli ya Golden Tulip.
   Msafara mzima wa timu hiyo wenye watu 24 wakiwemo wachezaji 19 utawasili nchini Jumanne (Februari 21 mwaka huu) na kufikia kwenye hoteli ya Holiday Inn.
  Februari 22 mwaka huu (saa 5 asubuhi) kutakuwa na mkutano wa makocha wa timu zote Jan Poulsen (Taifa Stars) na Le Roy (DRC) utakaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
  Wakati huo huo, kikosi cha Taifa Stars kilichotangazwa Februari 16 mwaka huu na Kocha Poulsen kesho (Februari 20 mwaka huu) kinaingia kambini jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi dhidi ya DRC na ile ya michuano ya AFCON 2013 dhidi ya Msumbiji ambayo itachezwa Februari 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DRC WAJA KWA MAFUNGU KUIVAA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top