• HABARI MPYA

  Sunday, February 26, 2012

  MBIO ZA VODACOM 5KM FUN RUN ZAFANA NDANI YA KILI-MARATHON MJINI MOSHI

  Baadhi ya washiriki wa mbio za kujifurahisha za”Vodacom 5 KM fun run”wakimaliza mbio zao nakujinyakulia zawadi mbalimbali.
   
   
  Na Mwandishi Wetu, Moshi

  Mbio za kujifurahisha za kilometa 5 za (Vodacom 5KM fun run) ambazo ni sehemu ya mbio za Kilimanjaro marathoni zimezidi kujizolea umaarufu kwa watu wengi wa rika tofauti kujitokeza kushiriki kwenye mbio hizo zilizofanyika jana/leo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

  Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mahusiano wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania ambao ndio wadhamini wa mbio hizo, Rukia Mtingwa katika mbio za mwaka huu jumla ya watu 10,000 wamejitokeza kushiriki kwenye mbio hizo tofauti na makadirio ya kawaida ya kupata jumla ya washiriki 5000 ambacho ndicho huwa kiwango cha juu .

  Mtingwa alisema wengi wa washiriki katika mbio hizo kwa mwaka huu zimetokana na uhamasishaji mkubwa uliofanywa na vyombo vya habari na mvuto wa mbio hizo ambazo huambatana na manjonjo mbalimbali Kutoka kwa washiriki wake na zawadi za kuvutia zinatolewa na Vodacom.

  Pamoja na mafanikio hayo Mtingwa alisema wao kama wadhamini wamepata changamoto kubwa katika mbio hizo hasa kwa mwaka huu kutokana na wakimbiaji wazoefu kujitosa kushiriki kwenye mbio hizo badala ya kuwaachia watu wengine ambao riadha sio fani yao .

  “Kwa kweli mwaka huu tumekumbana na changamoto hiyo ya wakimbiaji profession kushiriki kwenye fun run ambazo sisi tunaona ni maalum kwa watu ambao riadhi si fani yao kwahiyo kipindi kijacho endapo tutaendelea na udhamini wa mbio hizi itabidi tuifanyie kazi changamoto hii,”alisema Mtingwa .

  Aidha Mtingwa alisema changamoto ya kujitokeza washiriki wengi kwao ni faraja kubwa na watajipanga kukubaliana na haki hiyo ili kuendana na mazingira ya ukubwa wa mbio hizo kadiri watu watakavyokuwa wakijitokeza.

  Washindi wa mbio za jana/leo kwa upande wa wanaume ni Gailet Ismail ambaye alichukua na nafasi ya kwanza na kujinyakulia simu ya mkononi aina ya ZTE S- 501,muda wa maongezi wa Sh 20,000, modem ya intaneti pamoja na M-Pesa ya Sh 100,000.

  Brazil Boay alichukua nafasi ya pili na kuzawadiwa simu ,muda wa maongezi,modem ya intanert na M-Pesa ya Sh 80,000 wakati mshindi wa tatu alikuwa Fabiano Nelson ambaye naye alipata simu,muda wa maongezi,modem na M-Pesa ya Sh 60,000.

  Na upande wa wanawake washindi walikuwa ni Jackline Sakilu,Catherine Iranga na Natalia Elisante ambao nao walijishindia zawadi sawa na zile walizopata wanaume , washindi wengi kuanzia nafasi wanne hadi 10 pamoja na wshiriki walioweza kumaliza mbio hizo nao walipata zawadi mbalimbali kutoka Vodacom.

  Huo ni mwaka wa tano tokea Vodacom iwe mdhamini wa mbio za kilometa tano za kujifurahisha (Vodacom fun run) ambazo ni sehemu ya mbio maarufu za Kilimanjaro ambazo mwaka huu zimeadhimisha miaka 10 tokea kuanzishwa kwake .
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBIO ZA VODACOM 5KM FUN RUN ZAFANA NDANI YA KILI-MARATHON MJINI MOSHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top