• HABARI MPYA

  Tuesday, February 21, 2012

  YANGA, ZAMALEK HAIELWEKI ITACHEZWA WAPI

  UONGOZI wa mabingwa wa Misri, Zamalek umesema umeshtushwa na hatua ya Shirikisho la Soka la Misri(EFA) kufuta mechi za kimataifa za kirafiki za timu ya taifa ya nchi hiyo kwa kipindi cha mwezi mmoja na kudai kitendo hicho kimewafanya mpaka sasa wasijue sehemu ambayo pambano la marudiano kati yao na Yanga litafanyika.
  Kabla ya EFA kufikia uamuzi huo ulioelezwa umetokana na kulegalega kwa hali ya usalama nchini humo, Mafarao hao waliokuwa wamepanga kucheza mechi za kimataifa za kirafiki dhidi ya Kenya na Uganda.
  Kwa upande mwingine, Zamalek ilipanga pambano la marudiano dhidi ya Yanga lifanyike Machi 3 kwenye Uwanja wa Arab Contractor mjini Cairo.
  Meneja msaidizi wa timu hiyo, Ismail Youssef aliuambia mtandao nchini Misri kuwa wamekitafsiri kitendo cha EFA kama kutokuwepo kwa usalama wa kutosha nchini humo hivyo kuliweka pambano lao dhidi ya Yanga katika mashaka makubwa ya kutofanyika nchini humo.
  “Ni mshtuko kufutwa kwa mechi za kimataifa za timu ya taifa, ina maana Misri haiko tayari kuandaa mechi. Kinaliweka pambano la marudiano kati yetu na Yanga lililopangwa kuchezwa hapa katika hali ya mashaka.
  "Mpaka sasa haiko wazi kama tutacheza mechi ya marudiano Misri au la.
  “Nafikiri hakuna ulazima wa kuwaacha wachezaji wetu wajiunge na timu ya taifa, hii itatusaidia katika maandazlizi yetu ya Ligi ya mabingwa," alisema Youssef
  Awali, Zamalek ilikataa ombi lililowasilishwa kwao na Yanga ya kuchezwa mechi moja pekee, kufuatia janga la mauaji ya watu 74 lililotokea kwenye mji wa Port Said wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Misri ikihusisha timu za Al Masry na Al Ahly.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA, ZAMALEK HAIELWEKI ITACHEZWA WAPI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top